
Klabu ya wachezaji wa mchezo wa kuteleza kwenye mawimbi ya maji kwa kibao kijijini Bureh kilizinduliwa kama shirika lisilo la kiserikali ambalo nia yake ilikuwa kuimarisha mchezo huo nchini Sierra Leone na pia kutoa nafasi za kazi kwa watu wa kijiji hicho. Kwa sasa hii ndio klabu ya kwanza na ya kipekee ya aina yake Sierra Leone.

Hadi miaka mitatau iliyopita, wachezaji wa klabu ya Bureh hawakujua mbinu za mchezo huu zinazotumiwa na watu kwingineko duniani

Watu wengi kijijini humo walijifunza mchezo wa kuteleza kwa mawimbi ya maji wakitumia vibao walivyoazima kutoka kwa wageni waliokuwa wanatembelea bahari. Sasa klabu hii inamiliki vibao ambavyo hivikodisha kwa watu wanaotaka kuvitumia

Jahbez ambaye alikuwa mvuvi alikuwa mmoja wa walioanzisha klabu hiyo .'' Haikuwa kazi rahisi , wakati mwingine ungetoka kutafuta vibao wala hupati kitu. Sasa haya ni maisha mazuri kwangu.''

K-K ni mchezaji wa kwanza mwanamke wa kuteleza kwa mawimbi ya maji kwa kutumia vibao Siera Leone. ''Wengine wanaogopa. Hawajui kuogelea'' Lakini ikiwa utajitolea kujifunza , unaweza kufanya lolote. '' Anasema K.K
No comments:
Post a Comment