Ujenzi kuchukua siku nne
Watu 8,000 hawana makazi
Kwenda Dodoma ni kupitia Iringa, nauli zapanda.jpg)
Baadhi ya wananchi wa tarafa ya Magole Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, wakiwa hawana la kufanya baada nyumba zao kujaa maji.
Ujenzi wa daraja la Mto Mkundi wilayani Kilosa mkoani Morogoro ambalo lilikatika kufuatia mafuriko yaliyotokea juzi, ulianza jana huku watu zaidi ya 8,0000 wakikosa makazi kutokana na kuongezeka kwa maji.
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, alisema ujenzi utakamilika ndani ya siku nne huku Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akiwahakikishia wananchi waliokumbwa na mafuriko katika vijiji vya tarafa ya Mogole wilayani Kilosa kuwa serikali itafanya kila jitihada kuwapatia huduma muhimu ikiwamo chakula na hifadhi za muda.
Wakati Serikali ikifanya jitihada za ujenzi huo, watu zaidi 8,000 hawana mahali pa kuishi kufuatia mafuriko hayo yaliyotokea juzi na kusababisha kifo cha mtoto mmoja ambaye mpaka sasa hajafahamika jina lake.
Akizungumza katika eneo hilo, Waziri Magufuli alisema tayari wataalamu wa ujenzi wameweka kambi katika maeneo yaliyoathiriwa ili kurejesha miundombinu hiyo.
Alisema kuwa watalaamu whao kwa kushirikiana na kampuni ya Kichina ya CCECC inayojenga barabara ya Magole-Turiani watafanya kila linalowezekana kukamilisha kazi kwa wakati.
“Wataalamu wangu wameweka kambi hapa usiku na mchana kuhakikisha wanarejesha mawasiliano kwa haraka,” alisema Dk. Magufuli.
Alisema kuwa daraja hilo linatarajia kukamilika Jumapili huku akitaka magari yote kutumia barabara iliyoelekezwa na serikali.
Waziri Mkuu Pinda ambaye alitembelea eneo hilo jana, alisema Serikali inafanya kila jitihada kuhakikisha waathirika hao wanapata misaada huku ikifanya kila jitihada za kurejesha mawasilino ya barabara kati ya mikoa ya Dodoma na Morogoro.
Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wananchi waliopatwa na mafuriko katika kijiji cha Magole na kusisitiza kuwa serikali haitaacha kuwasaidia wananchi hao kwa kuwa chakula kipo cha kutosha na huduma nyingine.
Waziri Mkuu aliwaagiza viongozi wa mkoa kuchukua hatua stahiki kukabiliana na magonjwa ya milipuko yanayoweza kutokea kutokana na mafuriko hayo, ikiwamo kuwapeleka wataalamu wa afya katika eneo hilo.
Akizungumzia barabara na daraja la mto Mkundi ambalo linaunganisha mikoa ya Morogoro na Dodoma, alisema kuwa tayari amezungumza na wataalamu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kurejesha mawasiliano ndani ya siku tatu ili kuondoa adha ya usafiri.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, alitaja takwimu za awali kuwa ni zaidi ya watu 8,000 ambao wameathiriwa na mafuriko hayo ambao wanahitaji misaada ya chakula, nguo na mahema.
Alisema ameunda kamati maalumu ya kufanya tathmini ya kina ili kupata idadi kamili ya watu walioathirika na mafuriko hayo huku akiagiza watendaji wa vijiji kuwasilisha taarifa halisi za walioathirika.
Alisema kufuatia mafuriko hayo, Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Kitengo cha Maafa tayari imetoa misaada mbalimbali ikiwamo vyakula, mahema, mablankenti, vyandarua na maji pamoja na misaada mingine ya chakula kutoka kwa wadau.
KUFA KUFAANA
Kuharibika daraja katika eneo maarufu la Feri kumeleta neema kwa vijana wa vijiji vya Magole na Dumila kuendesha ujasiriamali wa muda ili kujipatia kipato kwa kuwavusha wananchi kutoka upande mmoja kwenda mwingine kwa gharama ya viwango tofauti kati ya Sh. 5,000 hadi 12,000. Bendera alisema kuwa watu hao wamekosa makazi baada ya nyumba zao kuharibiwa na nyingine kujaa maji, hali iliyowafanya kushindwa kuokoa vitu na vyakula.
Alisema kuwa idadi hiyo inaweza kuongezeka baada ya kufanyika kwa tathmini inayofanywa na kamati maalumu ya maafa ya Mkoa wa Morogoro.
“Tumeunda kamati maalumu ya maafa kufanya tathmini ya kina ili kupata idadi kamili ya watu waliokumbwa na maafa hayo, lakini kwa sasa taarifa za awali zinaeleza kuwa kuna zaidi ya watu elfu nane hawana makazi,” alisema.
Bendera alisema watu hao kwa sasa wanahitaji vyakula, mablanketi na sehemu ya muda kwa ajili ya kuhifadhiwa ili kuendelea na maisha yao.
Naye Ofisa Mfawidhi wa Sumatra mkoa wa Morogoro, Warukani Luhamba, alisema kutokana na kuharibika kwa barabara hiyo, zaidi ya malori 2,000 yamekwama katika eneo hilo.
Alisema malori hayo yamebeba bidhaa mbalimbali yakiwamo mafuta na kwamba kukwama huko kutaathiri uchumi wa nchi kwa kuwa barabara inayopitika sasa haichukui zaidi ya uzito wa tani 12.
Nao wananchi walioathirika na mafuriko hayo wamelalamikia kukosa huduma muhimu na kulazimika kulala nje.
MABASI YAPITIA IRINGA
Wakati huo huo, mabasi yanayofanya safari zake kupitia barabara ya Dodoma-Dar es Salaam jana yalilazimika kupitia barabara ya Iringa kufuatia kukatika kwa mawasiliano baada ya daraja kuu la Magole kusombwa na mafuriko kwa nauli ya Sh. 30,000.
Wakala Mkuu wa mabasi hayo mkoani hapa, Rashid Zuberi, alisema jana mabasi yote ya asubuhi yalipitia barabara hiyo kwa nauli ya Sh. 29,000
Alisema kuwa kwa mabasi ya Shabiby na Kimbinyiko baadhi yalishindwa kusafiri.
Aliiomba serikali kufanya jitihada za haraka ili kulipatia ufumbuzi suala hilo ili kuondoa usumbufu kwa abiria.
Mfanyakazi wa Shabiby, Mushi Abdul, alisema mabasi yao ya asubuhi mpaka saa tatu ndiyo yaliyoweza kusafiri, lakini la saa 5:30 lilishindwa na kuwarudishia nauli abiria.
Baadhi ya abiria waliozungumza na NIPASHE, walisema mabasi yaliyopita njia ya Iringa yaliwatoza nauli ya Sh. 30,000 huku ya kawaida wakilipa Sh. 20,000.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment