ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, January 26, 2014

MAUAJI COLUMBIA MALL NI KUTOKANA NA WIVU WA MAPENZI

Brianna Benlolo, 21, mmoja ya marehemu pamoja na mpenzi wake aliyeuawa nae walikuwa wanafanya kazi kwenye Mall hiyoColumbia.

Polisi wametaja majina ya watu watatu waliokufa siku ya Jumamosi January 25, 2014 ndani ya Mall ya Columbia iliyopo Haward County, Maryland na sababu ya vifo hivyo ni kutokana na wivu wa mapenzi baada Brianna Benlolo, 21, mkaazi wa College Park, Maryland., na Tyler Johnson, 25, mkaazi wa Ellicott City, Maryland kuuawa na Boy Friend wake wa zamani na baadae nae akajimaliza kwa risasi.  Briana na Tyler walisha chumbiana na walikuwa wafanyakazi katika duka la Zumiez lililopo ghorofa ya pili ndani ya Mall hiyo. Muaji ambaye alitambuliwa kwa jina la Darion Aguilar, 19 ambaye alikuwa mpenzi na Brianna siku za nyuma na msemaji wa Polisi amesema wanaamini muuaji alijilipua muda mfupi baada ya wao kuwasili ndani ya dkk 2 baada ya kupata simu kutoka kwenye Mall hiyo kuhusiana na mauaji hayo.
Tyler Johnson, 25 mchumba wa Brianna mmoja ya waliouawa.

4 comments:

Anonymous said...

Kumbe hata marekani kuna wachaga..

Anonymous said...

wachaga ndo kina nani?

Anonymous said...

jamani msicheza na mapenzi hata siku mmoja hajalishi ni mapenzi ya aina gani hujui mnapoachana na mwenzio roho yake inakuwaje ndo hapo anapoamu kulipiza kisasa achaneni kwa roho njema na kusameheyana na kuombeyana kheir other wise mambo kama haya kila leo tutayaona katika dunia hii hajalishi ni marekani au hata hap home tanzania

tusijifanye wababe katika mapenzi na wapenzi wetu

nasisitiza tena jamani tusifanye mchezo na mapenzi si yakufanyia mchezo ndo maana watu wanafanya vitu vya ajabu sana mpaka mtu unashangaaa


mpende akupendaye achana naye asiyekupenda kwa wema na amani si kumdharau au kumuona hafai kwa vile umepata kipya tuwe wastaarabu na kama binadamu si kuwa kama wanyama

ushauri wabureeee

Anonymous said...

Umenena wewe wa hapo juu. Mapenzi huchipua na kusinyaa. Ni kawaida sana tokea miaka hiyooo. Ustaraabu ni muhimu.