
Matatizo ya shingo ya kizazi (cervical incompetence) kutokana na maambukizi ya fangasi maeneo hayo. Kutoka kwa mbegu za kiume muda mfupi au saa kadhaa baada ya tendo ni dalili kuu ya tatizo hili. Pia mwanaume anapogonga shingo hii ya kizazi mwanamke huwa kama anatoneshwa kidonda. Hali hii ya mbegu kurudi nje husababisha mwanamke kutoshika ujauzito.
Kuwa na uvimbe kwenye mji wa mimba/mfuko wa uzazi (Uterus). Uvimbe huu kitaalam hujulikana kwa majina mengi lakini `fibroid` ni maarufu Zaidi. Huanza kama mbegu ndogo ya mchicha na hu kua kama boga kubwa. Mwanamke huongezeka ukubwa wa tumbo na baadaye huonekana kama ana mimba kubwa na watu hushangaa kwa nini hajifungui kipindi chote.
Maumivu wakati wa tendo hasa chini ya kitovu huashiria tatizo kwenye mirija ya uzazi. Yawezekana ikawa ni tatizo la mirija ya uzazi kujaa maji machafu kutokana na kuzaliana sana eneo hilo, tatizo ambalo hujulikana kitaalam kama Hyrosalpinx.
Kitu hiki husababisha mirija ya uzazi kuziba kwani maji haya huwa mazito, kitu ambacho husababisha mayai ya uzazi na mbegu za kiume kushindwa kupenya. Kutoshika mimba kwa mwanamke aliye kwenye ndoa au uhusiano kwa zaidi ya mwaka mmoja na anasikia maumivu ya aina hii ni kiashiria kikubwa cha tatizo hili.
Itaendelea wiki ijayo.
GPL
No comments:
Post a Comment