Na Faustine Ruta, Bukoba
TIMU ya Mbeya City leo imeanza msimu wa pili vyema baada ya kuifungia Kagera Sugar kwenye uwanja wao wa nyumbani kaitaba bao 1-0. Kipindi cha kwanza kilimalizika kikiwa hakuna timu iliyokuwa imeziona nyavu za mwenzake hivyo zikalazimika kwenda mapumziko zikiwa 0-0, Huku kipa wa Kagera Sugar Hannington akiwa hoi kwa kuumia mguu baada ya kuachia frii kiki na kushtuka mguu na kulazimika kutolewa nje katika kipindi hicho cha kwanza. Kipindi cha pili dakika ya 72 Mbeya City wamepata bao kupitia mchezaji wao Richard Peter aliyekuwa amevaa jezi no. 13 mgongoni.
Kikosi kilichoanza cha Mbeya City
Patashika kuutafuta mpira
No comments:
Post a Comment