Mahakama nchini Kenya imetoa hukumu ya kihistoria Jumatatu (tarehe 27 Januari) kwa jangili wa Kichina aliyekamatwa na pembe za ndovu, akiwa ni mtu wa kwanza kushtakiwa chini ya sheria kali mpya zilizotungwa mahsusi kukomesha vitendo vya ujangili, liliripoti Shrika la Habari la AFP
Tang Yong Jian, 40, alikiri makosa hayo ya kumiliki kinyume cha sheria na kuhusika na biashara haramu ya pembe za ndovu
pamoja na baada ya kukamatwa wiki iliyopita akiwa ameba pembe hizo zenye uzito wa kilo 3.4 katika mkoba wake alipokuwa anasafiri kutoka Msumbiji kuelekea China kupitia Nairobi.
Mchina huyo alipewa faini ya shillingi millioni 20 sawa (dola 233,000) au atumikie kifungo cha miaka saba jela. Ana siku 14 kukata rufaa kuhusu hukumu hiyo.
Chini ya sheria mpya ya kukabiliana na ujangili, kujihusisha na nyara za wanyama pori kunaweza kupelekea faini isiyo chini ya shilingi milioni 1 (dola 11,600) au kwa uchache kifungo cha miaka mitano jela, au vyote viwili.
Uhalifu wa kiwango cha juu kabisa dhidi ya wanyamapori - kuua wanyama walio hatarini - sasa kunaweza kupelekea kifungo cha maisha, na pia faini ya hadi shilingi milioni 20 (dola 233,000). --- Credit:Emmanuel Shilatu na Shirika la habari la Sabahi.
No comments:
Post a Comment