Naibu katibu Mkuu wa
CCM Bara Mh;Mwigulu Nchemba hii leo 27/01/2014 asubuhi amewasili Mkoa
wa Tanga akitokea Arusha kwenye Uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi mdogo wa
Udiwani kata ya Sombetini.Mh;Mwigulu Nchemba amekuwa kwenye ziara ya
Kichama ya Kuzindua kampeni za Uchaguzi wa Udiwani kata mbalimbali
Nchini,Akiwa ameanzia Mkoa wa Mtwara(Tandahimba),Mkoa wa
Manyara(kiteto),Mkoa wa Arusha(Sombetini) na hii leo ameingia Mkao wa
Tanga na Jioni ya Leo atakuwa Bagamoyo kwenye Uzinduzi wa Kampeni za
Udiwani Kata Kibindu.
Naibu
Katibu Mkuu licha ya kuendesha Ufunguzi wa Kampeni za Uchaguzi wa
udiwani,Pia amekuwa akifanya Vikao vya ndani vya Mkoa husika anaofika
kuzindua Kampeni.Vikao vya ndani vya Watumishi wa Chama Cha Mapinduzi
vimewa vikihusisha Makatibu wa Mikoa na Wilaya na Jumuia zake
zote.Ameshafanya Vikao hivyo Mkoa wa Mtwara,Manyara,Arusha,Hai,Moshi na hii
leo ameshatua Tanga kwaajili ya Kikao hicho cha Watendaji wa Chama Mkoa
wa Tanga.
Picha
hapa chini ni Kikao Kianchoendelea Muda huu Tanga cha Watumishi wa
ndani wa Chama kabla ya Kuondoka kuelekea Mkoa wa Pwani.
Naibu
Katibu Mkuu(Kulia) Mh Mwigulu Nchemba akisikiliza Utambulisho wa
Watendaji wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga wanaotambulishwa na
Katibu wa Mkoa wa Tanga wa CCM,Kshoto ni Mkuu wa Wilaya ya Korogwe
Mh;Mrisho Gambo.
Watendaji
wa Mkoa wa Tanga wa Chama Cha Mapinduzi wakitoa zawadi ya Mbuzi kwa
Naibu Katibu Mkuu kwa Kuteuliwa kwake kuwa Naibu waziri wa Fedha,Hii
inaonesha ni namna gani alivyomchapa kazi na anavyoaminika na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh;Jakaya Mrisho Kikwete.
Zawadi zinaendelea kwa Mh:Mwigulu Nchemba kwa Kuteuliwa kwake kuwa Naibu waziri wa Fedha.
Kikao
kimeshaanza na Kinaendelea sasa,Naibu katibu Mkuu anatoa Ujumbe
alioubeba kwa Watendaji wa Chama Cha Mapinduzi hapa Mkoa wa Tanga.
Picha zote na Habari Kwanza Blog
1 comment:
ndiyo hao tunayoongea mtu mmoja vyeo kumi, leo yupo kwenye chama na huyo huyo kwenye fedha
Post a Comment