
Ndege iliyobeba mwili wa marehemu Shekh Athumani Magee ikiwa imewasili uwanja wa ndege wa Musoma.

Mkuu wa Mkoa wa Mara John Tuppa akielekea kwenye ndege kuongoza waombolezaji.

Rubani wa ndege iliyoleta mwili wa marehemu Shekh Athumani Magee akielekeza namna ya kutoa jeneza.

Waombolezaji wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa Mara wakijipanga kupokea jeneza lililobeba mwili wa shek Athumani Magee.

Waombolezaji wakisubuli kuchukua jeneza lililobeba mwili wa marehemu sheik Athumani Magee baada ya kuletwa na ndege kutokea Dar es Salaam.
kwa picha na habari zaidi bofya soma zaidi

Gari maalum la JWTZ lililobeba mwili wa marehemu.

Waumini wa dini ya Kiislamu pamoja na wananchi wa Musoma wakiwa uwanja wa ndege.

Afidh Waziri mmoja wa watu waliokuja na mwili wa marehemu shekh Magee toka Dar es Salaam akiagana na rubani wa ndege.

Wananchi wa Musoma wakiwa uwanja wa ndege.

Mwili ukiondolewa uwanja wa ndege kuelekea nyumbani.

Msafara wa magari ukielekea nyumbani.

Msafara wa ukiwa njiani kuelekea nyumbani kwa marehemu shekh Magee.

Msafara ukiongozwa na bodaboda

Mkuu wa mkoa akiwasili nyumbani kwa marehemu shek Magee.

Mwili ukishushwa nyumbani.

Waombelezaji wakiwa nyumbani.

Shekh Athumani Magee alifikwa na mauti baada ya kugua kwa muda na mrefu na kupatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa Bugando kwa muda kabla ya kuhamishiwa Muhimbili kwa uangalizi zaidi na akiwa njiani kupelekwa nchini India kwa matibabu zaidi.
Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam waliokuwepo kwenye uwanja wa ndege Musoma wakiusubili mwili wa shekh Magee wamesema wamepata pigo kubwa kutokana na msiba huo kutokana na Shekh kuwa mstari wa mbele katika kuhimiza masuala ya dini.
Shekh wa mkoa wa Mara anatarajiwa kuzikwa kesho kabla ya swala ya adhuhur katika makabari ya Musoma Bus mjini Musoma.
INNAH LILLAH WAINNAH ILLAH RAJIUUN
HABARI NA PICHA KWA HISANI YA SHOMARI BINDA
No comments:
Post a Comment