Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
Stori: Imelda Mtema
MCHEKESHAJI maarufu Bongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amesema kama asingekuwa msanii basi angekuwa mfanyakazi wa mahakama.
Akistorisha na paparazi wetu juzikati, Steve Nyerere alisema kuwa kila msanii anatakiwa kujiuliza kama siyo kazi ya usanii angekuwa anafanya kazi gani lakini kwa upande wake yeye angekuwa mfanyakazi wa mahakama kwani anaipenda kazi hiyo.
“Huwa najiuliza mara kwa mara lakini siku zote naamini isingekuwa sanaa ningekuwa mfanyakazi wa mahakamani, napenda kuwapeleka watu lupango, kazi nzuri sana,” alisema Steve Nyerere.
No comments:
Post a Comment