Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond juu ya umuhimu wa kujifunza mauaji ya kimbari ya wayahudi ya mwaka 1933.
Na Mwandishi Wetu, MOblog Tanzania
Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) kimeendelea kutoa mafunzo na elimu juu ya umuhimu wa kukumbuka maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya ukombozi wa kambi za mateso ya Auschwitz kwa wanafunzi wa sekondari na shule za msingi nchini.
Akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond ya jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Afisa habari wa kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama amesema kwamba ni muhimu kwa kizazi na kizazi kujifunza madhara ya mauaji na maangamizi ya moto dhidi ya wayahudi yaliofanywa na askari wa kinazi wa Ujerumani.
“Ni muhimu kutoa mafunzo kwa vijana wakitanzania wa shule za msingi na sekondari ili wajue kwamba tofauti za rangi na za kidini hazina nafasi ya kutugawa kama binadamu,” amesema Nkhoma.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Diamond na Mlezi wao wakimsikiliza Bi. Ledama (hayupo pichani).
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama, akisoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataiafa katika siku ya kimataifa ya maadhimisho ya kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya maangamizi ya moto.
Nkhoma amesema kwamba binadamu wote ni sawa na tofauti za kipato au dini au rangi haziwezi tena kujenga chuki dhidi ya binadamu wengine kwa sababu wote kama binadamu tuna haki sawa mbele za mungu.
Wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond jijini Dar es Salaam, wakifuatilia sinema maalum ya mauaji ya kambi za mateso ya wayahudi mwaka 1933.
“Umoja wa Mataifa ulianzishwa kuzuia kila aina hii ya fazaa kutokea tena, lakini bado misiba kuanzia Cambodia hadi Rwanda mpaka Srebrenica inaonyesha kuwa sumu ya mauaji ya kimbari bado inatiririka,” ilisema taarifa hiyo.
Pichani juu na chini ni Wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond wakisoma baadhi ya machapisho ya Umoja wa Mataifa.




2 comments:
sijaelewa bado, kwanini tusiwafundishe watoto mauaji ya rwanda au burundi au kinachoendelea somalia mimi naona tuko more related and more applicable kuliko ya ulaya au tuwafundishe biashala ya utumwa.siajabu baadhi ya hawa watoto ni wanyarwanda.mimi nilisoma na watutsi walikuwa wanajiita wahaya.jirani zangu walikuwa wasomali.it is ok to know what happen in other part of the world,but at this moment than ever we need to teach our youth our history.
umenena ukweli mkuu hapo juu lakini kumbuka hii yote ni propaganda ili badaye watu wawaonehuruma hawa watu kama walivyokuwa wanawafanyia marekani kwa sababu wanaawazia watoto toka wadogo hawa wajui mauaji haya halafu baadaye wao waje watawale biashara zote bongo kama ilivyokuwa huku marekani halafu wanaambiwa eti they are blessed,my foot hii ni mwanzo pole pole wanaingia katika jamii ya kitanzania kama walivyoingia katima marekani utakuja kuniambia baada ya miaka 15 au 20.
ni kweli kwa mwenye akili kwa nini tusiwafundishe mauaji ya burundi,rwanda na somalia hawataki waafrica wajue histori hizo wanataka wao wajue historia za kwao ambazo hazina manufaa na jamii zetu halafu baadaye waje watucheke kwamba hatuna tunalolijua la kwetu ndo njama zao hizi
hakuna serikali tanzania na wakuu wao wanachojua ni kuteka mali za walala hoi
Post a Comment