Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Ahmed Msangi.
Wanafunzi 355 wa Shule ya Sekondari Wenda iliyoko eneo la Mbalizi Halmashauri ya Mbeya vijijini, wamenusurika kufa baada ya mabweni waliyokuwa wakiishi kuteketea kwa moto.
Hata hivyo, moto huo uliozuka ghafla, uliteketeza kabisa baadhi ya vitu vya wanafunzi hao.
Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Ahmed Msangi, alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi.
Mkurugezi wa shule hiyo, Fideles Daniel (54), ndiye aliyegundua mabweni hayo yakiteketea kwa moto saa 2:15 usiku. Aliongeza kuwa mabweni yalioathiriwa na moto huo ni mawili ya State House na Malcom X ambapo hakuna kitu kilichookolewa.
Aidha, alisema katika mabweni ya Kofi Annan na Marcus, moto ulidhibitiwa na kikosi cha Zimamoto cha Halmashauri ya Mbeya kwa kusaidiana na wanafunzi na wananchi wanaoishi jirani na shule hiyo kabla haujaleta madhara.
Kwa mujibu wa Kamanda Msangi, wakati mabweni hayo yakiteketea kwa moto, wanafunzi walikuwa katika vyumba vya madarasa wakijisomea.
Alisema kuwa chanzo cha moto huo bado hakijajulikana na thamani ya mali zilizoteketea vikiwamo vitanda 74 walivyokuwa wakilalia wanafunzi inaendelea kufanyiwa thamani.
Kamanda Msangi alitoa wito kwa wamiliki wa shule na taasisi nyingine kuhakikisha kwamba wanakuwa na vifaa vya kuzimia moto ili kukabiliana na matukio ya aina hiyo pindi yanapotokea.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment