Anastazia Anyimike, HabariLeo -- WATANZANIA waishio ughaibuni wameanza kushirikishwa kwa kupewa ajira serikalini, ikiwa ni njia kuwapa nafasi ya kuchangia maendeleo ya nchi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alisema hayo wakati wa ufunguzi wa semina kwa wakufunzi watakaotekeleza mradi wa kushirikisha Watanzania waishi o nchi za nje (Diaspora) katika kuchangia maendeleo ya Tanzania.
Membe alisema kwa miaka miwili iliyopita, Rais Jakaya Kikwete amekuwa akiwapa nafasi za uongozi Serikalini, Watanzania waishio nje ya nchi: “Kwa takribani miaka mwili, Rais (Kikwete) amekuwa akiwaajiri diaspora (Watanzania waishio nje ya nchi) ili kuonesha ulimwengu kuwa tunawajali,” alisema Waziri Membe. Alisema, “ Mfano mmoja ameajiriwa Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Rais Zanzibar na Mkuu wa Wilaya, lakini tutegemee watu wengi kupewa ajira ili kuchangia maendeleo ya nchi.”
Membe alisema katika mpango wa kutaka kushirikisha Watanzania waishi o nje kuleta maendeleo ya nchi, wamebaini
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alisema hayo wakati wa ufunguzi wa semina kwa wakufunzi watakaotekeleza mradi wa kushirikisha Watanzania waishi
Membe alisema kwa miaka miwili iliyopita, Rais Jakaya Kikwete amekuwa akiwapa nafasi za uongozi Serikalini, Watanzania waishio nje ya nchi: “Kwa takribani miaka mwili, Rais (Kikwete) amekuwa akiwaajiri diaspora (Watanzania waishio nje ya nchi) ili kuonesha ulimwengu kuwa tunawajali,” alisema Waziri Membe. Alisema, “ Mfano mmoja ameajiriwa Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Rais Zanzibar na Mkuu wa Wilaya, lakini tutegemee watu wengi kupewa ajira ili kuchangia maendeleo ya nchi.”
Membe alisema katika mpango wa kutaka kushirikisha Watanzania waishi
Watanzania wengi walio ughaibuni ni masikini na hawana kazi za maana, kutokana na kukosa uraia wa nchi husika. “
Tulichofanya ni kwenda kuzungumza nao kuangalia changamoto zinazowakabili, tulichobaini ni kuwa watu hao ni masikini na hawana uwezo wa kuchangia maendeleo, na pia hawana kazi za maana pamoja na kuwa na taaluma ambazo zingewafanya wapate kazi ya maana,” alisema.
Alisema nchi nyingine, raia wake walikwenda ughaibuni kama wakimbizi hivyo kupewa nafasi ya upendeleo ya kufanya kazi na kusoma, lakini Watanzaniawanashindwa kufanya hivyo kutokana na kukosa uraia wa nchi hizo. Alisema ufumbuzi wa tatizo hilo ni kubadili sheria ya Uhamiaji iruhusu Watanzania kuwa na uraia pacha.
“Tunashukuru mchakato wa Katiba umeliweka hilo,” alisema na kuongeza ana imani, ifikapo 2015 suala hilo litakuwa historia. Membe alitoa mfano wa nchi ambazo raia wake wanachangia uchumi kuwa ni Kenya, ambao wanachangia dola bilioni 1.6 kwa mwaka, Ghana dola bilioni 2.1 na Nigeria dola bilioni 3.5 kwa mwaka.
Aidha, Membe aliwataka wakufunzi wanaopewa mafunzo hayo, kuhakikisha wanatoa elimu kwa Watanzania wanaopinga mpango huo ili wajue kuwa kuishi ughaibuni siyo uhaini au usaliti bali ni njia ya kutafuta maisha.
“Tumefanya sensa ya kutambua Watanzania wanaoishi nje ya nchi, pamoja na kuwa bado haijakamilika mpaka sasa kuna Watanzania milioni 3.7,” alisema.
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), Damien Thuriaux alisema wamezindua mradi huo baada ya kupokea maombi ya msaada wa ufundi na fedha kwa Serikali ya Tanzania.
Alisema mradi huo umelenga kuimarisha uratibu miongoni mwa wizara kuhusu masuala ya wahamiaji, kuelewa njia ya kushirikisha Watanzania waishi o nje ya nchi, na kusaidia kutengeneza mtandao na itadhaminiwa na Mfuko wa Maendeleo wa IOM (IDF).
Tulichofanya ni kwenda kuzungumza nao kuangalia changamoto zinazowakabili, tulichobaini ni kuwa watu hao ni masikini na hawana uwezo wa kuchangia maendeleo, na pia hawana kazi za maana pamoja na kuwa na taaluma ambazo zingewafanya wapate kazi ya maana,” alisema.
Alisema nchi nyingine, raia wake walikwenda ughaibuni kama wakimbizi hivyo kupewa nafasi ya upendeleo ya kufanya kazi na kusoma, lakini Watanzaniawanashindwa kufanya hivyo kutokana na kukosa uraia wa nchi hizo. Alisema ufumbuzi wa tatizo hilo ni kubadili sheria ya Uhamiaji iruhusu Watanzania kuwa na uraia pacha.
“Tunashukuru mchakato wa Katiba umeliweka hilo,” alisema na kuongeza ana imani, ifikapo 2015 suala hilo litakuwa historia. Membe alitoa mfano wa nchi ambazo raia wake wanachangia uchumi kuwa ni Kenya, ambao wanachangia dola bilioni 1.6 kwa mwaka, Ghana dola bilioni 2.1 na Nigeria dola bilioni 3.5 kwa mwaka.
Aidha, Membe aliwataka wakufunzi wanaopewa mafunzo hayo, kuhakikisha wanatoa elimu kwa Watanzania wanaopinga mpango huo ili wajue kuwa kuishi ughaibuni siyo uhaini au usaliti bali ni njia ya kutafuta maisha.
“Tumefanya sensa ya kutambua Watanzania wanaoishi
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), Damien Thuriaux alisema wamezindua mradi huo baada ya kupokea maombi ya msaada wa ufundi na fedha kwa Serikali ya Tanzania.
Alisema mradi huo umelenga kuimarisha uratibu miongoni mwa wizara kuhusu masuala ya wahamiaji, kuelewa njia ya kushirikisha Watanzania waishi
3 comments:
hehehehehe hiyo ya uraia pacha imenichekesha. I thought he was smarter than that Sasa amesema watanzania ni masikini kwa vile hawawezi kufanya kazi za maana kwa vile hawana documents sasa kama mtu hana makaratasi huo uraia pacha utamsaidiaje? Kama mtu ana uraia wa nchi nyingine si anawea kwenda kufanya kazi kama TX?
Uraia wa nchi mbili watakaonufaidika ni wahindi, waarabu waliotumia pasi za TZ kuja huku ulaya na sio watanzania.
Wajamaica wana program inaitwa welcome back home or returning home. Ni program kwa wajamaica waliokaa nje kwa zaidi ya mika 10 na wanataka kurudi. Hivyo wanawatafutia kazi kabla hawajafungasha na kuondoka kutokana na professions zao.
Watu wengi wako radhi kubakia nje ya nje kwa ajili hawana uhakika wa kupata ajira wakirudi. Pamoja na elimu Tanzania ni lazima kumfahamu mtu ili upate kazi sasa hiyo inawafanya wakubali kuwa underpaid na kuweza kusogea polepole kuliko kurudi Tanzania na kuumbuka.
Wakumbuke watanzania wengi waliosoma na hawana kazi nchi za nje walipata elimu zao Tanzania. Wamemaliza vyuo vikuu vya Tanzania na hawakupata kazi wakakimbilia nje wakijua kua watapata kazi. Sasa kabla ya kufikiria watanzania walioko nje ni vizuri kusaidia na vijana wanaomaliza college nchini kwasababu nao wanasubiri kuondoka. Itakua kupishana tu hawa wanarudi.
Asante mheshimiwa Membe kwa kauli nzito na muafaka, tunaisubiri kwa hamu uamuzi wa katiba kuhusu swala zima la raia pacha kwani hatuoni kipingamizi na kuona WaTanzania ni wakimbizi sio> Nafasi nyingi sana zinaenda kwa watu baki, wakati waTanzania wapo na wanaweza. Mungu ibariki TZ na wadau wake.
Watanzania walio nje wameanzisha jumuia ya dunia nzima ili kwa pamoja wasaidiane na kukusanja fedha kuwekeza mabilioni nchini Tanzania ili kutoa ajira kwa kwa ndugu zao.Tovuli yao ni www.TanzaniaGlobalNetwork.Org
Post a Comment