
Watu 3 wamekufa baada ya kutokea kurushiana risani kariibu na duka la Sears lililopo ndani ya Mall hiyo ya Columbia karibu na upande unaouzwa chakula kwa mujibu ya polisi waliofika kwenye Mall hiyo baada ya kupata simu mbili tatu kutoka kwa watu tofauti wakielezea kusikia milio ya risasi iliyosababisha watu kukimbia kila upande kwa ajili ya kusalimisha maisha yao.
Tukio hilo lililotokea leo Jumamosi January 25, 2014 kuanzia saa 5 asubuhi msemaji wa Polisi amesema wanachofanya sasa hivi ni kujaribu kuwaondoa watu wote kwenye Mall na aliendelea kusema kwamba kati ya watu waliokufa inasemekana mmoja alikua mtuhumiwa aliyekuwa akifyatua risasi hizo.
No comments:
Post a Comment