Waziri wa Fedha, Saada Mkuya amekiri Serikali kuwa katika hali ngumu, lakini akasema kuwa mkakati uliopo ni kudhibiti matumizi ili yaendane na fedha iliyopo.
Waziri Saada alisema hayo kwa njia ya simu, alipotakiwa na Mwananchi Jumapili kujibu madai ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) juu ya kauli yake ya hivi karibuni aliyoitoa katika mkutano mjini Dodoma.
“Ni kweli nimesikia alichosema CAG na nadhani alimaanisha kudhibiti matumizi ya rasilimali kulingana na mahitaji. Siyo kwa Tanzania tu, nchi zote huwa zinazingatia matumizi ya rasilimali kulingana na mahitaji yaliyopo” alisema Saada na kuongeza:
“Sisi kama wizara tumejipanga kukusanya na kutegemea fedha zetu za ndani kupitia Mamlaka ya Mapato (TRA). Tunategemea misaada, lakini huwa inachelewa. Hata wakaguzi nao wanapaswa kuangalia hilo.”
Hata hivyo, Saada alisema kuwa Serikali ina fedha za kutosha kuendesha shughuli zake.
Alhamisi wiki hii CAG,Ludovick Utoh akifungua Mkutano wa pili wa Baraza la Wafanyakazi wa Ukaguzi nchini mjini Dodoma alisema, Serikali ya Tanzania iko hoi kifedha hivyo Bunge na Serikali lazima wajitathimini na kuongeza wanayo matumaini kutokana na ushauri ambao umekuwa ukitolewa na ofisi yake kufanyiwa kazi.
MWANANCHI
2 comments:
Namaswali kidogo; Kwanza kabla sijaweka hayo maswali lazima tujue unyeti wa wizara inayo enda kuongozwa, FEDHA. Uwezo wa kupambanua mambo ya fedha kwa kushirikiana na taasisi nyingine na za kimataifa.
Hii CV nimeiona hata kwenye website ya Bunge. kuna vitu vya kuwekea question mark kwenye hii CV na uwezo wake
Moja, haionyeshe shule aliyopatia masters degree, ADV Diploma wala certificate
Pili, amekili bado yupo anasoma chuo huria Dar. Kwa hiyo anasoma na kufanya intern kwenye wizara nyeti. Inakuwaje mtu aongoze wizara nyeti kama hii ilihari hajamaliza masomo.
Tatu, experience yake haieleweki. Huwezi mpa mtu wizara nyeti kama hii kwa shule na experience ya kuungaunga
Nne,High school kamaliza 1995. Courses for The Second Degree in Business (whatever this means) kafanya 2000 - 2002. Alikuwa wapi mika sita yote hiyo?
Haki ya mungu, hii ni cv kweli ya waziri wa Fedha? Mbona aibu? No experience,colleges hazieleweki,
Majanga haya!
Post a Comment