Mwenyekiti wa C C M. wa DMV Ndugu George Sebo(kushoto) ambaye alifuatana na Katibu wa Itikadi na uenezi Bi Salma Moshi (kulia)wakiwa nyumbani kwa wafiwa Bladensburg, Maryland wakikabidhi mchango kwa niaba ya tawi la CCM California. Ndugu George Sebo alisema mpendwa wetu Zainabu amefariki na kuacha pengo kubwa ndani ya CCM na huku familia yake ikiwa bado inamhitaji. Zainab atakumbukwa daima. Wengine katika picha ni Dullah wapili toka kushoto Mume wa marehemu na Mdogo wa marehemu Ngalu Buzohera, PiaMwenyekiti akizungumza na Mume na Mdogo wa marehemu aliwaomba kuwa na moyo wa subira baadae Mwenyekiti na Katibu waliongea na mama wa marehemu Tanzania na kumueleza rambirambi hizo lutoka CCM California na wamewakabidhi Dullah na Ngalu kwa niaba yao Tanzania. Mama wa Marehemu alishukuru sana kwa mchango huo na ushirikiano mkubwa ulonyeshwa.

1 comment:
Ni jambo zuri sana kushikamana wakati wa matatizo na kutoa rambirambi. Menyezi Mungu awape wepesi wafiwa katika kipindi hiki kigumu. Na Mwenyezi Mungu amlaze ndugu yetu mahalai pema peponi.
Ningependa kufanya masahihisho kidogo kuwa hakuna CCM California ila kuna CCM Bay Area. California ni jimbo lenye msongamano wa watu zaidi ya milioni 38. Bay Area ni sehemu ndogo tu ya jimbo la California.
Post a Comment