ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, February 6, 2014

HOFU YA VYETI FEKI SERIKALINI



  • WATUMISHI WOTE SASA KUHAKIKIWA VYETI VYAO
  • ASKARI WALIOVITUMIA KUPANDA VYEO KUKIONA
Na Heri Shaaban
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, limetoa mwezi mmoja kwa watumishi wake wote  kuwasilisha vyeti vyao ili viweze kufanyiwa uhakiki ili kubaini kama kuna vyeti feki.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Job Masima, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati wa Mafunzo ya Elimu ya Hifadhi ya Jamii yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA).
Alisema kuanzia leo, watumishi wote waliopo chini ya Wizara hiyo watapaswa kuwasilisha vyeti vya vyuo walivyosomea."Natoa mwezi mmoja kuanzia leo hadi Januari, wawasilishe yeti vyao wizarani viweze kukaguliwa...baada ya ukaguzi tutafuatilia maeneo waliyosomea ili kubaini kama kuna
askari wanaotumia vyeti feki," alisema.

Alisema askari ambao watabainika kutumia vyeti feki na kupata vyeo wakiwa kazini, watashushwa vyeo ambapo lengo a ukaguzi huo ni kuwataka watumishi hao kusomea katika vyuo vinavyotambulika na Serikali si vya mitaani.

Aliongeza kuwa, mpango huo pia utawahusisha watumishi ambao wamesomeshwa na Wizara ambao nao watatakiwa kwasilisha vyeti vyao upya.Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Bi. Irene Isaka, aliwataka watumishi wa Wizara hiyo kujiunga na Mifuko ya Hifadhi za Jamii kwa ajili ya kuweka mafao yao.

Alisema kuna mifuko mingi hivyo kila mtumishi anaweza kuchagua wowote anaopenda kujiunga nao ili uweze kumsaidia dhidi ya matukio yasiotarajiwa.Matukio hayo ni pamoja na maradhi, ulemavu, kustaafu kazi,kuacha kwa hiari au kwa lazima. Akizungumzia changamoto zilizopo katika sekta hiyo, alisema takwimu zinaonyesha wananchi walio katika sekta rasmi wanakadiriwa kufikia milioni 1.5 ndio wananufaika na sekta hiyo.

Majira

No comments: