William Zelothe Stepehen akiwa ndani ya ndege aina ya Airbus A319.
William Zelothe Stepehen ni Mtanzania wa Kwanza Mmasai aliyepewa ithibati ya kuiongoza ndege aina ya Airbus A319 punde tu baada ya kupokea mafunzo ya urubani yaliyodhaminiwa na shirika la ndege la fastjet. Alipata mafunzo hayo nchini Uingereza kwa muda wa takriban miezi miwili na amerudi nchini Tanzania hivi karibuni. William alikulia Olosipe jijini Arusha ambapo ni nyumbani kwa wazazi wake.
William anafananisha anavyojihisi anapoiongoza ndege ya Airbus A319, na wakati akiwa katika nyumba nzuri ya kifahari na ya kisasa; anaielezea ndege ya Airbus A319 kama ndege iliyo imara na ambayo imewekewa mifumo mingi ya usalama. Kwa maneno yake mwenyewe, anasema “Ndege ya Airbus inakulinda kweli kweli, kama unaifahamu vyema”
William amewahi kusomea usimamizi wa wanyama pori; alipata mafunzo ya urubani kwa mara ya kwanza kule Florida Aviation Academy nchini Marekani mwaka 2006 ambapo alipata leseni yake ya usafirishaji kwa ndege. Ingawa ana umri mdogo, ana uzoefu wa masaa 3,053 ya kuongoza ndege.
Kumwajiri rubani huyu mtanzania mwenye miaka 28, ni mojawapo ya jitihada za fastjet za kuhakikisha kuwa kampuni hiyo inaajiri watendaji wazawa waliobobea katika fani hiyo hapa nchini. Mikakati yao ya kuajiri pia ni mojawapo ya wajibu wao mpana wa kuwekeza nchini Tanzania. Kwa kila rubani aliyepokea mafunzo, fastjet imetumia gharama inayokadiriwa shilingi 49,546,400 hela za kitanzania ambayo ni sawa na 31,027 dola za kimarekani.
Fastjet ni shirika jipya la ndege la nauli nafuu Afrika ambalo lilipata umiliki wa FLY540 na kwa mantiki hiyo likazindua kampuni ya kwanza ya usafiri wa ndege ambalo linazingatia bajeti. Fastjet, ambayo inaungwa mkono na mwanzilishi wa Lonrho na easyGroup Bwana Stelios Haji Ioannou, imetambulisha nauli za kiwango cha chini hadi kiasi cha Tsh32,000 bila kujumlisha kodi ili kuwawezesha mamilioni ya watu ambao walikuwa wameshindwa kusafiri kwa ndege, kuweza kusafiria ndege kwa mara ya kwanza na kuendelea kutumia ndege mara kwa mara. Tangu kuzinduliwa kwake mwezi Novemba 2012, shirika hili la fastjet limewasafirisha zaidi ya watu 70,000 na asilimia 99.7 ya safari za ndege zikisafiri katika muda uliopangwa.
Credit:Matukio na Vijana
Credit:Matukio na Vijana
4 comments:
Hivi kweli kuna umuhimu wa kusema kuwa ni mmasai wa kwanza kurusha ndege? Kuna makabila mengi tu Tanzania hawana marubani. Mbona mnawadhalilisha wamasai hivyo? Inaelekea rubani mwenyewe amejieleza hivyo shauri ya kimbelembele.
Kweli ukiambiwa ni mshamba,usishangae nikwamba watu wameona ushamba wako. Nisifa kuona mmsai wakwanza anaendesha ndege....Rais mweusi wakwanza kuiongoza Marekani,nk. Hivyo wamasai wamepata Rubani wakwanza nchini...nimtanzania mwenye kabila la kimasai.na wakwanza Tanzania kurusha ndege kubwa akiwa na umri mdogo.....pendeni makabila yenu jamani...ndiyo maana mnawachukia Wahaya,Wachagga kwasababu wanapenda makabila yao.....
Keep it up Will. Thank you for making your parents proud. Hongera mama Willy.
Mdau uwe na utaratibu wa kuchuja habari. Ukabila umepitwa na wakati. Habari hapa ni ipi? Mmasai kuendesha ndege? Na makabila mengine wameshaendesha wataandikwa lini? Research yako umetumia sample ipi? Huyu ni mmasai wa kwanza kuendesha ndege wapi?
Post a Comment