ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, February 9, 2014

Promotion of Solar Energy for Long-term Growth in Tanzania

Mafundi wa Ageco Energy wakifunga solar moja ya nyumba jijini Arusha hizi karibuni

Vincent Mughwai, CEO wa Ageco Energy, anasisitiza umuhimu wa matumizi ya nishati mbadala "alternative energy" kwa nchi ya Tanzania na bara zima la Afrika badala ya kutegemea umeme wa nguvu za maji (hydro power) kwani maji yanapungua kila siku na mito inakauka kwa kasi kubwa. Anasisitiza kuwa tusipojipanga vizuri na kuendelea kutegemea nguvu za nishati zenye kikomo (hydro, gesi, n.k) tutashtukia tuko kwenye janga kubwa la ukosefu wa nishati ya kutosha. Kwamba tafiti mbali mbali zinaonyesha kuwa asilimia 67% ya watu duniani watakuwa na tatizo kubwa sana la maji ifikapo 2030. Kwa nchi yetu tayari hali ni mbaya. Ndio maana hatuna umeme wa uhakika kwasababu mabwawa ya Mtera na Kidatu hayana maji tena ya kutosha kuendesha mitambo ya umeme. Wanasayansi wanatabiri pia kuwa baada ya miaka kama 50 hivi gesi asilia nayo itakuwa imepungua sana huko ardhini, hivyo tusipokuwa makini na tukaelekeza nguvu zote katika uwekezaji wa umeme wa gesi asilia huko Mtwara tunaweza kuja kupata shida siku za usoni. Nishati endelevu za mionzi ya jua, upepe, bio-mass n.k hazitakwisha. Jua litakuwepo siku zote, upepe vivyo hivyo. Katiba mpya iweke msisitizo wa kuendeleza nishati mbadala.

Kampuni ya Ageco inatoa huduma ya umeme wa sola kwa nchi nzima ya Tanzania. Tunafunga umeme vijijini na mijini, kwa watu wasio na umeme na wale wenye umeme wanaohitaji backup badala ya kutumia genereta.

Tuko Ubungo, Riverside, DSM. Tovuti http://www.agecoenergy.com/; Emailinfo@agecoenergy.com Simu +255758-733333 na +255652-222064.

3 comments:

ulotu said...

Sawa kabisa ushauri mzuri. Je unaweza kutupa gharama za kufunga solar kwa muhtahsari?

Anonymous said...

Ushauri mzuri. Je unaweza kutupa bei za solar installation kwa ufupi?

Anonymous said...

Niliishawasiliana na huyu kaka kwa ajili ya nyumba ya wazazi wangu ipo Dar na alinipa estimation nzuri sana milioni 5 hivi but that was 2 years ago na inategemea unataka kutumia kwa nini taa only, taa na kupika, plus AC. Inadetermine ukubwa wa mashine ya kurushia umeme. Kwa kifupi is very affordable na one time investment na baada ya hapo hakuna monthly luku wala bills. Its worth it.