Raisi Yoweri Museveni.Rais Yoweri Museveni wa Uganda ametoa matamshi makali dhidi ya Rais Barack Obama wa Marekani akimtaka akome kungilia masuala ya ndani ya Uganda.
Matamshi hayo makali yamekuja baada ya Rais wa Marekani kutishia kuwa uhusiano wa nchi yake na Uganda utaharibika iwapo Rais Museveni atasaini na kuufanya kuwa sheria muswada wa kupinga vitendo vichafu vya kujamiiana watu wa jinsia moja.
Agusia Kushirikiana na Russia.
Rais Museveni amesema, atashirikiana na Russia iwapo Marekani itaendelea kuingilia masuala ya ndani ya Uganda na kuongeza kama ninavyomnukuu:
“Russia imekuwa ikifanya shughuli zake barani Afrika tangu mwaka 1917 yaani kwa zaidi ya miaka 100. Ninataka kushirikiana na Russia kwa sababu hawachanganyi siasa zao na siasa za nchi nyingine.” Mwisho wa kunukuu
Ameongeza kuwa: “Ukiona mtu anaingia ndani ya nyumba ya mtu mwingine basi jua kuna tatizo. Hapa ni nyumbani petu. Huwezi kumuona mtu mwenye upaa kama mimi hivi ndani ya nyumba yake na kuanza kumpangia afanye unavyotaka wewe. Rudi kwenu!” Alisema Rais Museven.
Credit:Matukio na Vijana blog
2 comments:
Bravo mzee Museveni kwa kuliweka hili very clear.Sisi bado tupotupo kwanza..
Nadhani Museveni kisha zeeka na kupoteza akili. Kuikana marekani is suicidal to him. Amesahau kuwa Marekani inamsaidia katika vita dhidi ya waasi in Northern Uganda? Museveni like other neighbors are not happy kwa sababu Rais O aliitembelea TZ only katika ziara yake iliyopita and ignored them. Anataka Warusi? go ahead Mr. Museveni, watakufilisi na kukuuzia mizinga ya karne ya kumi na saba!
Post a Comment