Msemaji wa kundi la kigaidi la al-Shabab la nchini Somalia amesema kuwa, wapiganaji wa kundi lake wanapanga mikakati ya kudhibiti tena maeneo yote ya Somalia ukiwemo mji mkuu, Mogadishu.
Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na kanali ya Aljazeera ya Qatar, Ali Dheere amesema kujiondoa wapiganaji wa al-Ahabab katika miji kadhaa ya Somalia hakupaswi kuonekana kama pigo bali ni mbinu ya wapiganaji hao ya kujipanga upya. Amesema kundi lake ambalo limetangaza mfungamano na mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda, halitasalimu amri.
Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia alisema siku chache zilizopita kwamba kundi hilo litaangamizwa kufikia mwisho wa mwaka huu.
Magaidi wa al-Shabab wiki iliyopita walishambulia Ikulu ya Rais mjini Mogadishu na kusababisha vifo vya watu 14. Wamesema mashambulizi hayo yalikuwa onyo kwa serikali kwamba kundi hilo bado lina nguvu ya kushambulia sehemu yoyote ndani na nje ya Somalia.
Chanzo, kiswahili.irib.ir/habari
No comments:
Post a Comment