ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 26, 2014

BALOZI ALIPOTEMBELEA SISTER CITY DURHAM, NORTH CAROLINA

Balozi Liberata Mulamula alikiwasili na kupokelewa na mwenyenyeji wake Rais wa sister city Bw, Brady Sulle siku ya Jumamosi March 22, 2014 alipotembelea Sister City Durham, North Carolina siku alipofanya ziara NC kwa mwaliko wa Jumuiya ya Watanzania North Carolina(UTNC) wa pili kushoto ni Afisa Ubalozi Switebert Mkama.
Mhe, Balozi Liberata Mulamula akipata maelezo kutoka kwa mhandisi wa Durham city Nd, Harold Byrd (kulia) kuhusu matumizi ya lori la taka ambalo limetolewa na sister city kwa matumizi ya kuzolea taka jijini Arusha.
Mhe, Balozi Liberata Mulamula akishuka kutoka kwenye lori ambalo alilifanyia ukaguzi.
Hilo ndilo lori ambalo limetolewa na sister city kwa matumizi ya kuzolea taka kwenye jiji la Arusha.
Mhe,Balozi Liberata Mulamula akibadilishana mawazo na mwanzilishi wa sister city Durham, NC na Arusha, Tanzania Bi, Dorothy Borden.
Makamu wa Rais wa sister city Durham, NC na Arusha, Tanzania Bi, Gwen Bukmen katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Liberata Mulamula.
Picha ya pamoja kutoka kushoto ni mwanzilishi wa sister city Durham, NC na Arusha, Tanzania Bi, Dorothy Borden, mwenyekiti UTNC Bwn. Geoffrey Lepana, Makamu wa Rais wa sister city Durham, NC na Arusha, Tanzania Bi, Gwen Bukmen, Afisa Ubalozi Switebert Mkama, Mhe. Balozi Liberata Mulamula, mhandisi wa Durham city Bwn, Harold Byrd, Bwn. Tony Nturu na Rais wa sister city Bw, Brady Sulle

1 comment:

Anonymous said...

Tanzania kwa kupenda vya bure, hela zote inatupwa kwenye katiba ambayo haionekani lakini kununua wenyewe hatukumbuki.

Tanzania ina hela nyingi sana tuache kupenda vya bure.