BAADA
ya mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kupitia kundi la vyama vya siasa,
Mchungaji Christopher Mtikila, kutishia kufungua kesi katika mahakama ya
kimataifa kuzuia vikao vya Bunge hilo, ameambiwa ni ruksa kufanya
hivyo.
Mchungaji
Mtikila ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP) alieleza
kusudio hilo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa,
akidai Bunge hilo ni batili kutokana na wajumbe wake kuteuliwa na mtu
mmoja ambaye ni Rais Jakaya Kikwete.
Akielezea
tishio la mjumbe huyo, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, alisema
ni haki yake kufanya hivyo na kwamba mahakama ndiyo itakayotoa uamuzi.
Source: Kamkara E. / Tanzania Daima

1 comment:
Huyu nae mcheza movie walimuingiza huko kwenye bunge kufanya nini?wanamjua sk zote ni mtu wa matukio, toka atoe songi lake la Magabacholi basi amekuwa mtu wa vituko tu.
Post a Comment