ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, March 1, 2014

CHADEMA YAENDELEA NA KAMPENI ZAKE ZA UCHAGUZI JIMBO LA KALENGO MKOANI IRINGA

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema taifa, John Heche, akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Lumuli, wakati wa kampeni za kumnadi mgombea wa ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga kupitia chama hicho, Grace Tendega uliofanyika kijijini hapo jana.
Meneja wa Kampeni za mgombea ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Alphonce Mawazo, akimwelezea mtoto Zakina Miwela, anayesoma darasa la pili katika Shule ya Msingi Lumuli, ambaye ni mtoto wa kiongozi wa CCM wa kijiji hicho, anavyoonekana bila viatu na sare zake kuchanika, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini hapo jana.
Meneja wa Kampeni za mgombea ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Alphonce Mawazo na mgombea, GraceTendega, wakizungumza na akinamama wa kijiji cha Lumuli, katika kikao maalumu baada ya mkutano wa kampeni, zilizofanyika kijijini hapo jana.
Mgombea wa CHADEMA akipokelwa Lumuli

kwa hisani ya Jiachie Blog

3 comments:

Anonymous said...

kumuonyesha motto hivyo ni abuse....sio sawa kabisa...hivi Tz kwanini hakuna sharia....mimi sio ccm,chadema wala sina chama naongelea tu habari ya huyu mtoto

Anonymous said...

WALLAHI HAWA WATU THEY HAD NO RIGHT TO HUMILIATE THAT CHILD IN THAT MANNER.KHA JAMANI MBONA SISI WATANZANIA TUKO HIVI?KWA KWELI HAKUNA CHAMA KITAKACHO SHIKA MAMLAKA AMBACHO KITAWEZA KULETA MABADILIKO YOYOTE. NI SISI WENYEWE KWANZA TUJIBADILISHE.

Anonymous said...

Hivi kuna ubaya gani kuwaonyeni ni jinsi gani viongozi wetu wasivyokuwa na uchungu na maisha ya hao watoto...kuweni wakweli....jamii yetu inateseka mno hasa wazawa....funguka.