Timu ya mafundi ya ukarabati na upanuzi wa mitambo ya Ruvu Juu wakiwa kazini katika Ofisi ya Mitambo hiyo, mkoani Pwani.
Kaimu Meneja wa Mtambo wa Ruvu Juu, Mhandisi Deusdedit Rwegasira (Aliyevaa fulana la mistari) akiwaonesha Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango video ya namna miundombinu ya maji inavohujumiwa na baadhi wananchi wasiofuata taratibu zilizowekwa za kwa kujiunganishia maji kiholela.
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikikagua maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa mitambo ya Ruvu Juu ilipofanya ziara ya ukaguzi katika Mtambo huo uliopo mkoa wa Pwani.
Meneja wa Mtambo wa Ruvu Chini, Mhandisi Emmanuel Makusa (Kushoto) akiwaonesha Wataalamu wa Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango mashine nne mpya zilifungwa na Serikali hivi karibuni walipofanya ziara ya ukaguzi katika Mtambo huo uliopo mkoa wa Pwani.
Viongozi wa msafara wa wataalam wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Bibi Florence Mwanri (Wapili Kushoto) na Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla), Prof. Longinus Rutasitara (Watatu Kulia) wakionesha eneo la kusafishia maji katika Mtambo wa Ruvu Chini walipokuwa katika ukaguzi wa mtambo huo. Kushoto ni Mratibu wa ziara hiyo, Bibi Salome Kingdom.
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikikagua bomba lenye uwezo wa kusafirisha lita milioni 360 za maji kwa siku wakati walipokuwa kwenye ukaguzi wa mitambo ya Ruvu Chini. Anayewaonesha ni Meneja wa Mtambo wa Ruvu Chini, Mhandisi Emmanuel Makusa (Wapili Kulia).
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Mtambo wa Ruvu Chini, Mhandisi Emmanuel Makusa (Watatu kushoto) kwenye lenye uwezo wa kusafirisha lita milioni 360 za maji kwa siku wakati walipokuwa kwenye ukaguzi wa mitambo ya Ruvu Chini.
Mafundi wakiendelea kulaza mabomba yatakayotumika kusafirishia maji kutoka Mitambo ya Maji ya Ruvu Chini mpaka kwenye Tanki la kuhifadhia maji lililopo Chuo Kikuu cha Ardhi jijini Dar es Salaam. Mpaka sasa mafundi hao wameshasambaza mabomba kwa umbali wa kilomita takribani 29 kati ya kilomita 55. Kazi hii inatarajiwa kukamilika mwezi Juni, mwaka huu.
Na
Saidi Mkabakuli
Tatizo
la muda mrefu la uhaba wa maji ya uhakika linalowakabili wakazi wa mkoa wa Dar
es Salaam na mikoa mengine inayohudumiwa na mitambo ya maji ya Ruvu Juu na Ruvu
Chini sasa litakuwa historia kufuatia uwekezaji unaofanywa na Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kukarabati na kupanua mitambo hiyo.
Hayo
yalibainika wakati Timu ya Ukaguzi wa
Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipofanya ziara ya
ukaguzi wa utekelezaji wa ukarabati na upanuzi wa mitambo hiyo iliyopo mkoa wa
Pwani.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti Mhandisi Deusdedit Rwegasira na Mhandisi Emmanuel Makusa
ambao ndiyo wasimamizi wa mitambo hiyo, walisema kuwa hali ya ukarabati wa
mitambo hiyo inakwenda kwa kasi na inatarajiwa kukamilika kwa wakati, hivyo
kutoa ishara njema ya kumaliza tatizo sugu la maji kwa mkoa wa Dar es Salaam na
Pwani.
Mhandisi
Rwegasira ambaye ni Kaimu Meneja wa Mtambo wa Ruvu Juu aliambia timu hiyo ya
ukaguzi wa miradi ya maendeleo hadi kukamilika kwake mtambo wake utakuwa na
uhakika wa kusafisha na kusambaza takribani lita milioni 100 kwa siku.
Akizungumzia
hali ya ukarabati huo, Mhandisi Rwegasira alisema kwamba mpaka sasa Mkandarasi
wa mradi huo ameshaanza kazi ya upanuzi wa mitambo hiyo pamoja na kukarabati
mitambo ya zamani. Aliongeza kuwa kwa mujibu wa mkataba waliouingia Mkandarasi
anawajibika kuongeza mabomba ya usammbazaji kutoka Ruvu Juu hadi Kimara,
kuboresha na kuongeza sehemu za kusafishia maji, kukarabati mashine za kuvutia
na kusambazia maji.
Aliongeza
kuwa Mkandarasi anawajibika kuongeza idadi ya mashine za kuvutia na kusambazia
maji ili kufikia lengo hilo kusafisha na kusambaza lita milioni 100 kwa siku.
“Mkandarasi
ameshaanza kazi ya kukarabati mitambo yetu ili kutuongezea ufanisi katika
kutekeleza uzalishaji wa kutosha wa maji bila kuharibu miundombinu yetu, pia
ameanza upanuzi wa mitambo ili kuongeza uzalishaji kama mkataba unavyosema,”
alisema Mhandisi Rwegasira.
Kwa
upande wake Mhandisi Makusa ambaye ni Meneja wa Mtambo wa Ruvu Chini alisema
kwamba mpaka sasa mradi wa upanuzi na ukarabati wa mitambo yake umefikia
aslimia 98 ya malengo iliyoazimiwa.
Mhandisi
Makusa alihakikishia timu hiyo ya ukaguzi kuwa kufikia mwezi Juni mwaka
huuwa mtambo wake utakuwa na uwezo wa
kuzalisha lita milioni 270 kwa siku ambazo zitasambazwa katika mkoa wa Dar es
Salaam na vitongoji vyake kupitia njia ya Ruvu Chini hadi kwenye Tanki la
kuhifadhia maji lililopo Chuo cha Ardhi jijini Dar es Salaam.
Mhandisi
Makusa alisema kuwa mradi uliokuwa ukitekelezwa kwenye mtambo wa Ruvu Chini
ulijumuisha ujenzi wa jengo la kuhifadhia mashine nne mpya za kusambazia maji,
ambapo mpaka sasa mashine mbili zimeshaanza kufanya kazi.
Aliongeza
kuwa Mkandarasi aliwajibika kutengeneza jengo jipya la kuchujia maji pamoja na
machujio yake manne na kutanua bwawa la kutulizia maji.
“Tunashukuru
sana Serikali kwa kusimamia vyema mkandarasi katika kutekeleza kazi hii kwa
wakati maana inatupa nguvu ya kuongeza uzalishaji hadi kufikia lita milioni 270
kwa siku,” alisema Mhandisi Makusa.
Ukarabati
wa Mtambo wa Ruvu Chini ulifanywa kwa ushirikiano kati wa Kampuni ya Spencon na
Ms Degremont.
Akizungumza
wakati wa ziara hiyo, kiongozi wa Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi
ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri anayeshughulikia Huduma za Jamii
na Maendeleo ya Idadi ya Watu, alisema kuwa shabaha ya ukaguzi wa miradi ya
maendeleo inachagizwa na ari ya Serikali ya Awamu ya nne katika kuhakikisha
kuwa wananchi wote wa Tanzania wanafikiwa na huduma bora na za uhakika ikiwemo
huduma ya maji safi na salama.
Aliongeza
kuwa kwa kutambua hilo eneo la maji limewekewa mkazo katika Mpango wa Maendeleo
wa Miaka Mitano.
“Maji
ni moja ya eneo la kimkakati katika kipaumbele cha kwanza cha Mpango wetu wa
miaka mitano ambapo uwekezaji mkubwa wa miundombinu hasa uwekezaji mkubwa
katika miundombinu ya nishati, usafirishaji, TEHAMA, maji safi na maji-taka na
umwagiliaji yamewekwa kwa lengo la kumnufaisha kila Mtanzania,” alisema.
Vipaumbele
vingine vilivyoainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2011/12 –
2015/16 wenye dhana ya kufungulia fursa za ukuaji wa uchumi Tanzania ni pamona
na kilimo, ambapo shabaha imewekwa katika kuleta mapinduzi ya kilimo ili
kuwezesha kujitosheleza kwa chakula na kuuza ziada nje ya nchi; kukuza
uzalishaji wa mazao yenye thamani kubwa; kuongeza uzalishaji wa mazao ambayo ni
malighafi ya viwandani; kuboresha ufugaji na uvuvi; kukuza kilimo cha misitu;
na kuhuisha ubora wa bidhaa zote za kilimo ili kukidhi viwango na mahitaji ya
soko.
Pia,
maendeleo ya viwanda, hasa vile vinavyotumia malighafi zinazopatikana hapa
nchini: viwanda ambavyo msingi wake ni mazao ya kilimo, mifugo, samaki; na
rasilimali misitu; viwanda vinavyoongeza thamani ya madini; viwanda vikubwa vya
mbolea na saruji; kanda maalum za kiuchumi zitakazokuwa na viwanda vya
kutengeneza bidhaa kwa ajili ya soko la ndani na lile la kikanda pamoja na
viwanda vya kieletroniki na vile vinavyohusiana na TEHAMA.
Vingine
ni pamoja na maendeleo ya rasilimali watu na ujuzi kwa kutilia mkazo maendeleo
ya sayansi, teknolojia na ubunifu na kuimarisha mafanikio yaliyopatikana katika
upatikanaji wa huduma za jamii; na uendelezaji wa huduma za utalii, biashara na
fedha.
Serikali imeaandaa Mpango wa
Maendeleo wa Miaka Mitano ukiwa na lengo la kuwa na mfumo madhubuti wa
kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Mpango huu utadumu kwa mwaka
2011/12 - 2015/16 na utakuwa wa kwanza
katika mfululizo wa mipango mitatu
itakayotekelezwa kwa awamu. Lengo la Dira ni kuibadili Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa
kati ifikapo 2025.
2011
– 2016 dhana ya kufungulia fursa za ukuaji wa uchumi Tanzania Vipaumbele hivyo ni: (i) miundombinu hasa
uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya nishati, usafirishaji, TEHAMA, maji safi
na maji-taka na umwagiliaji; (ii) kilimo, kwa shabaha ya kuleta mapinduzi ya
kilimo ili kuwezesha kujitosheleza kwa chakula na kuuza ziada nje ya nchi;
kukuza uzalishaji wa mazao yenye thamani kubwa; kuongeza uzalishaji wa mazao
ambayo ni malighafi ya viwandani; kuboresha ufugaji na uvuvi; kukuza kilimo cha
misitu; na kuhuisha ubora wa bidhaa zote za kilimo ili kukidhi viwango na
mahitaji ya soko; (iii) maendeleo ya viwanda, hasa vile vinavyotumia malighafi
zinazopatikana hapa nchini: viwanda ambavyo msingi wake ni mazao ya kilimo,
mifugo, samaki; na rasilimali misitu; viwanda vinavyoongeza thamani ya madini;
viwanda vikubwa vya mbolea na saruji; kanda maalum za kiuchumi zitakazokuwa na
viwanda vya kutengeneza bidhaa kwa ajili ya soko la ndani na lile la kikanda
pamoja na viwanda vya kieletroniki na vile vinavyohusiana na TEHAMA (iv)
maendeleo ya rasilimali watu na ujuzi kwa kutilia mkazo maendeleo ya sayansi,
teknolojia na ubunifu na kuimarisha mafanikio yaliyopatikana katika upatikanaji
wa huduma za jamii; na (v) uendelezaji wa huduma za utalii, biashara na fedha.
tangu kufunguliwa kwake tarehe 8 Desemba 1976
mtambo huo uongezaji wa jengo jip
“
wakati wa ukaguzi huo mmoja wa
katika
kutambua changamoto zinazowakabili wakazi wa mkoa huo, Mpango wa Maendeleo
uliweka bayana uanzishaji na uendelezaji miradi ya maendeleo ili kutoa huduma
za kijamii kwa Watanzania wote.
No comments:
Post a Comment