ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, March 25, 2014

ELIMU YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE JUU YA UFUGAJI NYUKI YAANZA KUFANYIWA KAZI KWA VITENDO

Baadhi ya Mizinga ya Nyuki katika Kikundi cha Mshikamano Katika Kijiji cha Iyayi Wilayani Wanging'ombe
Na Gabriel Kilamlya Wanging'ombe 
Wanachama wa Kikundi cha Ufugaji Nyuki cha Mshikamano Kilichopo Katika Kijiji cha Iyayi Wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe Kimetajwa Kukabiliwa na Uhaba wa Mtaji wa Kuongeza Mizinga Ya Nyuki Ili Iweze Kufikia Mizinga Mia Tano.
Hadi Sasa Kikundi Hicho Kimefanikiwa Kumiliki Mizinga 225 Ya Nyuki Ambayo Imetolewa na Wafadhili Katika Kuwakwamua Wananchi Kiuchumi.

Akizungumzia Hali ya Kikundi Hicho Mwenyekiti wa Kikundi Bwana S-----Sungura Amesema Kuwa Kikundi Hicho Tangu Kianze Mwezi April 17 Mwaka 2013 Kimefanikiwa Kupa Fedha Kiasi Cha Zaidi ya Shilingi Milioni Mbili Kutokana na Mavuno Ya Asali.

Akizungumzia Suala la Ufugaji Nyuki Katika Kikundi Hicho Mkuu wa Mkoa wa Njombe Capteni Mstaafu Asseri Msangi Amewataka Wataalamu wa Nyuki Kuhakikisha Wanasaidiana na Wananchi Katika Kuhakikisha Wanafuga Kitaalamu Ili Waweze Kupata Asali Nyingi Zaidi.

Aidha Msangi Amewashauri Wananchi Hao Kuboresha Maeneo Ya Ufugaji wa Nyuki Hao Kutokana na Hali Ya Mvua Zinazoendelea Kunyesha Ili Kuongeza Kiwango cha Uzalishaji wa Asali.

No comments: