Stori: Mussa Mateja na Shakoor Jongo
LILE gari aina ya Toyota Land Cruiser V8 alilokuwa akitanua nalo staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ liko sokoni linapigwa bei.
Gari hilo linalomilikiwa na pedeshee maarufu Bongo, Mohammed Kiumbe ‘Chief Kiumbe’ limewekwa sokoni baada ya staa huyo kuchemsha kutoa fedha za kulinunua pamoja na kupewa muda wa kufanya hivyo.
Awali, iliripotiwa kuwa gari hilo ni mali ya Diamond ambaye alikuwa akitamba nalo kila pembe ya Jiji la Dar huku akijinasibu kwamba amelishalipa fedha za kutosha kwa ‘Big Boss’, Chief Kiumbe.
Wengi waliamini na kumweka Diamond au Sukari ya Warembo katika matawi ya juu kutokana na kumiliki gari hilo lenye thamani kubwa na lililojaa vikorombwezo vingi ndani yake.
Picha za Diamond akiwa ndani ya gari hilo zilionekana kwenye magazeti huku akikaririwa kwamba analimiliki kihalali gari hilo aina ya Toyota Landcruiser V8 lenye thamani ya shilingi milioni mia moja na laki moja (100,100,000).
Siku chache zilizopita, Chief Kiumbe alimnyang’anya Diamond gari hilo kwa kile kilichodaiwa kuwa staa huyo alishindwa kutoa ‘mpunga’ wa kulinunua pamoja na kukaa nalo kwa muda mrefu.
Baada ya hapo gari hilo likapotea machoni mwa watu kwa kutojulikana lilipokuwa limefichwa ingawaje ilidaiwa kuwa Chief Kiumbe alikuwa ameliweka stoo.
Mapaparazi wa Risasi Mchanganyiko walilitafuta gari hilo kwa udi na uvumba, ndipo walipobaini kwamba lilikuwa limewekwa sokoni katika yadi moja iliyopo maeneo ya Kijitonyama, Dar likipigwa bei.
Waandishi wetu walifika katika yadi hiyo na kujifanya wanunuzi na kuambiwa kuwa gari hilo lilimshinda Diamond.
“Hili gari lina vitu vingi vizuri, ukiwa na ‘sensa’ ndipo unapoweza kuondoka nalo kwa sababu halitumii funguo, bila hivyo huwezi, Diamond ameshindwa kulinunua,” alisema jamaa aliyekutwa katika yadi hiyo.
Waandishi hao walitajiwa bei na kupewa nafasi ya kulikagua gari hilo kila kona, hatimaye waliondoka ndani ya yadi hiyo wakiahidi kurudi na mkwanja ili kufanya kile kilichomshinda Sukari ya Warembo.
GPL
2 comments:
Bongo Bwana!! This dude was Just Bragging the other day on the news how rich he was, with estimate of one billion Tsh= to $625,000. I never heard Mr Dewji bragging how much US billion dollars he has. Kweli maskini akipata matako hulia mbwata!
Jamani tuulizeni sisi tulio huku mbele tuwaambie magari ya thamani wanayomiliki mastaa yenye thamani ya mamilioni na wala husikii wakijigamba gari hilo ukiagiza japani second hand sio used yani ni kama jipya tu hata milioni hamsini hazifiki tatizo ni kodi kubwa hapo bandarini kwetu kweli usipojua mambo ni sawa na usiku wa giza hata chakavu kwenye minada ya serikali ukitafuta unaweza kulipata sio gari laku kuthamanishwa kihivyo waabongo badilikeni acheni mambo ya kuna watu hapo bongo wana maferari posche na magari mengine ya kifahari wala huwasikii kujitapa na utawaona kwa nadra barabarani kweli masikini akipata ni shida Bwana mdogo diamond achana na mambo ya magari nunua ardhi ,jenga nyumba za biashara kama geust house, fremu za maduka kanunue mashamba ya miti ya kuchana mbao wekeza bwana mdogo pesa hairudi mara mbili mambo ya wanawake na magari achana nayo umri unakwenda na siku zinavyokwenda wanaibuka machipukizi wengine wakali kwenye GAME waulize kaka zako wakina MB DOG Mr. Nice wakuambie Bwana mdogo tulia fanya vitu vya maana
Post a Comment