.jpg)
Uongozi wa Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam umesema uko tayari kuilipa timu ya AS Cannes ya Ufaransa kiasi cha Euro 33,000 sawa na Sh. milioni 73.1 za Tanzania ili kumrejesha beki wake wa zamani, Shomary Kapombe, katika msimu ujao wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara.
Akizungumza na gazeti hili jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya timu hiyo, Zacharia Hanspope, alisema klabu imeshafanya mazungumzo na wakala wa mchezaji huyo, Denis Kadito, na kukubaliana kulipa kiasi hicho cha fedha.
Hanspope alisema kwa sasa wanaendelea kufanya mazungumzo na Kapombe ili kufikia makubaliano ya kiasi cha mshahara watakachompa beki huyo wa zamani wa Polisi Morogoro.
“Ni kweli tumeshazungumza na Cannes na wamekubali tuwalipe fedha ili Kapombe arejee Simba," alisema kwa kifupi kiongozi huyo.
Aliongeza kuwa, endapo watafikia makubaliano Kapombe atasaini mkataba wa miaka mitatu ya kuichezea klabu hiyo ambayo sasa iko katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.
Simba ilimtoa Kapombe kwa mkopo kwenda AS Cannes katikati ya mwaka jana akiwa bado ana mkataba na klabu hiyo lakini alipofika Ufaransa alianza kupatiwa matibabu na mafunzo maalum ambayo yanadaiwa kuigharimu klabu hiyo kiasi hicho cha fedha.
Kapombe yuko hapa nchini tangu mwaka jana alipoitwa kwenye kikosi cha timu ya Tanzania (Taifa Stars) kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Zimbabwe uliofanyika Novemba mwaka jana.
Habari nyingine zinaeleza kuwa Kapombe aliliandikia barua Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) akiomba ruhusa ya kufanya mazoezi na timu ya Azam lakini shirikisho hilo lilikataa kujihusisha na ruhusa hiyo.
Chanzo kingine kinaeleza kuwa uongozi wa Azam umekuwa ukimuwinda nyota huyo kutaka kumsajili lakini amekuwa akiwakwepa na hata amekataa kufanya mazoezi ya timu hiyo yenye uwanja na vifaa bora vya mazoezi.
Kapombe amekataa kuzungumza lolote kuhusiana na hatma yake akieleza kwamba wakala wake ndiye anayepaswa kuzungumza.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment