Mafundi wa Kampuni ya ujenzi wa daraja la Kigamboni wakisuka nondo katika moja ya nguzo zitakazoshika daraja hilo
Meneja wa Mradi wa ujenzi wa daraja la Kigambonio Bw. Lin Tao kutoka kampuni ya China Railway Construction Engineering Group and Major Bridge Co. Ltd (CRCEG-MBEC
JV) akionesha jinsi ambavyo daraja la
kigamboni litakavyoonekana baada ya kukamilika. Kulia kwake ni Mratibu wa Mradi kutoka Wizara ya Miundombini Bw. Hussein Mativila. Daraja hilo kutoka Kurasini mpaka Kigamboni takribani kilometa moja litakuwa na njia sita kwa ajili ya magari. Daraja hili linajengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF)

Timu
ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
wakipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa daraja la kigamboni kutoka
kwa Bw Lin Tao (katikati) kulia kwake (mwenye tai nyekundu) ni Naibu
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayesimamia Kongane ya Sekta za
Uzalishaji. Wa kwanza kulia (mwenye suti nyeusi) ni Meneja wa Mradi
kutoka NSSF, Bw Karimu Mataka
Naibu
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayesimamia Kongane ya Sekta za
Uzalishaji, Bw. Maduka Kessy akisisitiza jambo wakati wa ziara ya
kukagua ujenzi wa daraja la Kigamboni. Mbele yake ni Menaja wa Mradi
kutoka Kampuni ya ujenzi wa daraja hilo (CRCEG-MBEC JV)
Moja
ya nguzo inayosukwa katikatika ya maji ya bahari huku kukiwa na bomba
la pembeni linalotoa maji nje ya eneo linalosukwa nondo na zege kali.
Mhandisi wa Mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni, Aldelsomond Elthag kutoka Arab Consulting Engineers (katikati)
akifafanua jambo kwa Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bw.
Maduka Kessy (mwenye tai nyekundu), kulia kwake ni Mhandisi Omari
Athumani kutoka Tume ya Mipango wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa
daraja hilo.
Picha zote: Joyce Mkinga,
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
No comments:
Post a Comment