ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, March 15, 2014

MEMORIAL WEEKEND SASA KUFANYIKA DMV, NEW YORK NA DMV KUPAMBANA KWA MARA YA KWANZA RATIBA KAMILI HII HAPA

New York Dream Team (NYATI)
Timu ya DMV
Kuanzia May 23- 25, 2014 Vijimambo Blog inakuandalia bonge la party, siku tatu za kula raha, nyama choma na mechi ya mpira iliyokua ikisubiliwa kwa hamu kati ya New York na DMV ni wiki ya memorial Weekend sasa kufanyika DC jiji la watunga sheria kwa nguvu zote. Tega sikio ratiba kamili itafuata.

IJUMAA May 23, 2014 kuanzia saa 3 usiku mpaka saa 9 alfajirii  ni Oldskul Night kama wewe ni kijana wa zamani sio usiku wa kukoza Pata Oldskul hapo chini ujikumbushekumbushe mambo yatakavyokuwa
Dj Luke The Mix Master III from Luke Joe on Vimeo.

JUMAMOSI May 24, 2014 Mechi ya Mpira DMV a New York kuanzia saa 10 jioni mpaka saa 1 usiku baadae usiku wa White International Party Dress all white

JUMAPILI may 25, 2014 kuanzia saa 10 jioni nyama choma Meadowbrook park na usiku Reggae Night

Three Night and two days to Party  address 4306 Georgia Ave, NW, Washington, DC 20011

Tutazidi kuwajuza zaidi kadri siku zinavyokaribia


Vijana wa New York wako tayari kwa ajili ya Memorial weekend baada ya majingambo na DC kuingia mitini. Safari hii DC wenyewe wamekubari mpambano huo wa nguvu na vijana wa New York siku hiyo ya Memorial weekend. Vijana wa New York wameshaanza kufanya mazoezi kwenye theluji siku hiyo moto utawaka ndani ya DC.
Team inadamu mchanganyiko na vijana wako tayari kutoa doze kwa DC Memorial weekend huko DC.
Hapa ni kisima cha skills Vijana wako mto moto
Rafa a.k.a the rock city kiatu kibaki mpira uende....!!
Ny Ebra bado yumo na timu yake ya New York...Hapa akijifua kupunguza kitambi hili awe fit kwa mpambano huo unaosubiriwa kwa hamu na pande mbile hizo.

3 comments:

Anonymous said...

Nawapenda sana Wabongo wa DMV mko very stress free. Mnajumuika sana wenzetu siyo Kama Huku dirty South kazi majungu tu. Nani Hana hiki na anafanya nini nk especially wanaume wambeya kulikoni. Anyway keep it up DMV.

Unknown said...

Polen weee

Anonymous said...

I luv the Jarusaleem song Luke -You got it what it takes for a DJ. Stay humble broda! See you in May..