Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Bi. Zuki Njalai Mihyo (kulia, aliyesimama) akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya yalioandaliwa na GTI. Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Bi. Zuki Njalai Mihyo (aliyesimama) akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya yalioandaliwa na GTI.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya. Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Bi. Zuki Njalai Mihyo (aliyesimama) akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya yalioandaliwa na GTI. Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya.
MKUU wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Bi. Zuki Njalai Mihyo leo jijini Dar es Salaam amefungua mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya yaliyowashirikishwa washiriki kutoka katika mikoa ya Dar es Salaam, Lindi, Pwani na Morogoro.
Akizungumza katika hotuba yake ya ufunguzi wa mafunzo hayo yanayofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Jinsia kilichopo eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam, Bi. Zuki Mihyo alisema kutokuwepo na misingi imara ya kutetea, kulinda na kudumisha demokrasia iliyojengwa kwenye misingi ya usawa wa kijinsia inayo tambulika Kikatiba kumechangia uwepo wa tatizo la unyanyasaji wa kijinsia nchini.
Alisema tatizo la unyanyasaji wa kijinsia licha ya kuwapata watu wa jinsia zote, limekuwa likiwaathiri zaidi wanawake na watoto wa kike tofauti na ilivyo kwa wanaume na watoto wa kiume katika jamii, hivyo kushauri kuna kila sababu ya kupambana na mifumo kandamizi inayochangia hali hiyo.
"...Wanawake na watoto wa kike mara nyingi wamekuwa wakifanyiwa ukatili huu na wanaume au wavulana ambao wanaweza kuwa ndugu zao wa karibu, marafiki na hata wenzi wao," alisema Mkuu huyo wa chuo cha GTI kilichopo chini ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP)
Mmoja wa watoa mada wa mafunzo hayo, Geoffrey Chambua (aliyesimama katikati) akizungumza na washiriki wa mafunzo.
No comments:
Post a Comment