Mahakama ya Wilaya ya Musoma.
Mwanamke mmoja amehukumiwa kifungo cha miaka mitano na miezi sita jela na Mahakama ya Wilaya ya Musoma, mkoani Mara, baada ya kupatikana na makosa ya kutoa matusi na kushambulia askari polisi wawili waliokuwa wanataka kumkamata.
Aliyekumbwa na adhabu hiyo ni Mary Jumanne, mkazi wa mjini Musoma, ambapo pia ameamriwa kuwalipa fidia ya Sh. 100,000 kila askari.
Hukumu hiyo imetolewa juzi na Hakimu Mwandamizi Richard Maganga, wa Mahakama ya Wilaya ya Musoma.
Awali, imedaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashitaka wa serikali, Jonas Kaijage, kuwa mshitakwa huyo alitenda kosa hilo Machi 3, mwaka huu.
Kaijage alisema kuwa mshitaikiwa huyo aliwashambulia na kutoa lugha ya matusi askari polisi wawili, PC. Hamis na WP. Kuruthumu kutoka ofisi ya afisa upelelezi wa mkoa wa Mara, waliokuwa wamekwenda kumkamata akikabiliwa na kosa jingine la kutoa lugha ya matusi.
Alisema kuwa baada ya polisi hao kutaka kumkamata ndipo mwanamke huyo alipowatukana na kisha akamshambulia askari wa Kuruthumu na kumsababishia maumivu mwilini mwake.
Mshitakiwa huyo alikiri kutenda makosa hayo huku akiomba mahakama hiyo impunguzie adhabu, ombi lililotupiliwa mbali na mahakama hiyo.
Hakimu Maganga alisema kuwa ametoa adhabu hiyo ili liwe fundisho kwa mshitakiwa huyo na kwa watu wengine wenye nia ya kudhalilisha watumishi wa serikali wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao.
Kabla ya hukumu hiyo kutolewa mwendesha mashitaka huyo aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa kwa madai kuwa ni mdhohefu wa makosa hayo.

CHANZO: NIPASHE
1 comment:
Kosa la kutukana siyo la kumfunga RAIA miaka 5:( hawa mahakimu wamekuwa miungu watu? Majitu yanaiibia serikali mamilioni lakini yanafungwa miaka 2 ..askari wawili mtuhumiwa mmoja mnasema amewapiga kivipi? Aliwashinda nguvu kivipi? Wewe hakimu muogope muumba wako ktk majukumu yako ..miaka 5 nikumharibu siyo kumfunza au ni kwa sababu hakuwa na cha kukuhonga?
Post a Comment