.jpg)
Mwanasiasa mkongwe na mjumbe Bunge la Katiba, anayewakilisha kundi la waganga wa kienyeji,Kingunge Ngombale Mwiru.
Video ya Kingunge na Kificho wakiongelea hotuba ya Warioba kwenye mahojiano na TBC1 mjini Dodoma
Mwanasiasa mkongwe na mjumbe Bunge la Katiba, anayewakilisha kundi la waganga wa kienyeji, Kingunge Ngombale Mwiru, ameichana Rasimu ya Katiba kuwa haina mipango madhubuti ya kuinua uchumi badala yake ni mtandao wa viongozi kugawana madaraka.
Kingunge aliyasema hayo juzi bungeni kwenye semina ya wabunge wakati Mwanasheria Mstaafu wa Kenya, Seneta Amos Wako, alipozungumza kuelezea uzoefu wa nchi yake kwenye mchakato wa kupata katiba mpya.
Kabla ya kutoa kauli hiyo, Kingunge alitaka kujua uhusiano wa katiba za nchi na maendeleo yake, akidai kuwa baadhi ya mataifa ya Afrika yalipata uhuru miaka zaidi ya 50 iliyopita na hayana maendeleo ya kuridhisha licha ya kuwa na katiba.
Alisema nchi hizo ziko nyuma kiuchumi na ni tegemezi ukilinganisha na mataifa ya Ulaya na Asia ambayo yamepiga hatua kimaendeleo licha ya kuwa wote wana katiba.
“Nilidhani katiba ni dira na maendeleo, nchi zote zina katiba, lakini inakuwaje sisi tuna katiba lakini tunabaki nyuma kimaendeleo? alihoji Kingunge.
Katiba za nchi za Kiafrika zinatilia mkazo suala la kugawana madaraka badala ya kuzungumzia maendeleo ya kiuchumi, jambo ambalo linasababisha kuendelea kubaki duni.
“Hata katiba tuliyoletewa hapa bungeni juzi mimi naiona kama ni mtandao wa kugawana madaraka, haizungumzii maendeleo ya uchumi, nauliza wenzetu wa Asia katiba zao pia hazizungumzii uchumi? Alihoji Kingunge.
Kingunge alisema kwa kuegemea zaidi kwenye kugawana madaraka, makundi mbalimbali ya kijamii yameendelea kuwa na hali duni za kimaisha kutokana na kukosa maendeleo
Aliwataja wakulima, wafugaji na wavuvi kuwa wamebaki nyuma kimaendeleo kwa muda mrefu na hali zao mpaka sasa hazitofautiani na zilivyokuwa enzi ya ukoloni.
“Sasa hapa tumepewa kazi ya kuunda katiba, nimepitia rasimu tuliyoletewa, nimeona haizungumzii makundi makubwa ya watu katika nchi yetu ambayo tumeyaweka kando tangu tulipopata uhuru kama wakulima, wafugani na wavuvi,” alisema Kingunge.
Rasimu ya Katiba iliyoletwa bungeni kwa mujibu wa uchambuzi wake imejaa maneno mazuri ya haki za binadamu, utawala bora na mengine mengi ambayo hayana tija kwa uchumi wa taifa.
Akijibu maswali ya Kingunge, Wako alisema ndiyo sababu ya wabunge hao kukusanyika Dodoma kwa ajili ya kutunga katiba mpya.
“Hayo aliyoyasema Mzee Kingunge ndiyo yanayotufanya tuwepo hapa, sisi ndio wenye jukumu la kutunga katiba nzuri yenye mwelekeo mzuri wa kukuza uchumi wananchi na taifa kwa ujumla,” alisema Wako.

CHANZO: NIPASHE
2 comments:
Nimekubali kweli wazee ni dhahabu...mie nilikua na hamu sana huu muungano ufe lakini baada ya kuwasikiliza hawa wazee wetu nimebadilika kabisa maana wameongea kwa busara kubwa kwa mtu yyt kuelewa manufaa ya huu muungano wetu...hongereni sana Mzee Kingunge Ngombale Mwiru na Mzee Ameir Kificho nyie ni lulu kubwa sana kwa nchi yetu...I'm very proud of you!!
Mdau wa UK
tokeni ...hamkuupa Warioba ...mwelekeo ... amebuni yeye mwenyewe wHere to GO LEO MNAMLAUMU
MTALAANIWA
AMEIFANYA KAZI YAKE VYEMA NA WASAIDIZI WAKE
TUTAJUA MWISHO
MAMBO NDO KWANZA YANAANZA
Post a Comment