ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 19, 2014

NIMCHEZAJI ANAELIPWA PESA NYINGI KULIKO MCHEZAJI YEYOTE KWA SASA TANZANIA

Emmanuel Okwi ni mchezaji ghali kuliko mchezaji yeyote Tanzania kwa wachezaji wa kigeni na wa ndani. Thamani yake imewafunika wachezaji wazawa katika timu ya Yanga. Kwenye nafasi yake  yaushambuliaji kuna Tegete na Javu lakini kutokana na ujio wake wachezaji hao wamekuwa bechi kama wachezaji wa akiba. Kwa mtazamo wangu mimi sidhani wachezaji wetu wazawa wamezidiwa uwezo na Okwi kwani wachezaji wote wa Afrika Mashariki na kati hawapishani sana katika uchezaji. Ni jukumu la kocha tu kuwa na mbinu za kujua mchezaji gani anaweza kucheza nafasi anayoweza kuimudu na kuongeza mbinu kidogo tu za kitaaluma. Okwi kwa gharama za pesa anazolipwa hadi sasa sijaona ubora wake na kashindwa hata kuifungia Yanga katika michezo miwili ya ligi ya nyumbani tukiacha hile ya kimataifa. Tunawahitaji akina Tegete, Javu na wengine wakaze misuli na wafanye vizuri katika nafasi zao kuliko kuwalipa mapesa wachezaji wenye uwezo sawa na wazawa.
Wapenzi wa Yanga na viongozi wakimpokea Okwi kwa mbwembwe.
Okwi akitambulishwa makao makuu ya Yanga Jagwani
Wapenzi wa Yanga wakiwa wameshika jezi yenye jina la Okwi swali ni Je  wapenzi wa Yanga wanakipata kile walichokuwa wanakitarajia kutoka kwa Okwi kwa faida ya timu yao?. 

No comments: