Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mjumbe Maalum wa Rais wa Afrika Kusini Mhe. Maite Nkoana-Mashabane, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nvhi hiyo Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Mjumbe Maalum wa Rais wa Afrika Kusini Mhe. Maite Nkoana-Mashabane, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nvhi hiyo Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Picha na Ikulu
UNITED
REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE,
THE
STATE HOUSE,
P.O. BOX
9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumapili, Machi 16,
2014, amepokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini.
Ujumbe huo wa Rais
Zuma umewasilishwa kwa Rais Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini,
Mheshimiwa Maite Nkoana-Mashabane wakati mama huyo alipokutana na kufanya
mazungumzo na Rais Kikwete, Ikulu, Dar Es Salaam.
Mara baada ya
kuwasilisha ujumbe huo, viongozi hao wamejadili masuala yanayohusu uhusiano
kati ya Tanzania na Afrika Kusini na masuala ya kikanda ambako nchi zote mbili
ni wanachama wa Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Mheshimiwa
Nkoana-Mashabane amendoka nchini mara baada ya kuwa amewasilisha ujumbe huo kwa
Rais Kikwete.
Imetolewa na;
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
16 Machi,2013



No comments:
Post a Comment