Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania Addo Novemba akisisitiza Jambo kwa Waandishi wa Habari hii leo.
Rais
Wa Shirikisho la Muziki Tanzania Ndugu Addo Novemba Mwasongwe hii leo
amezungumza na Vyombo vya Habari kuhusu Kuimarika kwa Shirikisho la
Muziki kwa Kuongeza Idadi ya Viongozi kwenye Shirikisho wakiwamo Wazee
wa Kwaajili ya Ushauri ndani ya Shirikisho,Pia Ombi la Shirikisho kwa
Serikali kuhusu Mchakato wa Katiba Mpya kuthamini nafasi ya sanaa
hususani Muziki kwenye Umiliki wa Kazi za Wananmziki,Mwisho namna
Shirikisho lilivyojipanga Kuanza kufanya kazi za Kijamii.Wataanza na Kampeni ya Okoa Mama na Mtoto.
Rais wa SMT Addo Novemba Mwasongwe akisisitiza Jambo hii leo Kwa Waandishi wa Habari.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari Ndugu Addo Novemba amesema"Kufuatia kikao
walichokaa Vyama Vyote vya Muziki Tar.7/03/2014 kuzungumzia namna
wanavyoweza Kujaza nafasi za Uongozi ambazo bado hazikuwa na Watu,Pia
Kuongeza Wajumbe wa Shirikisho kutokana na Wajumbe kadhaa wa awali
kutofika ama kuto shiriki kabisa shughuli za shirikisho,Walifikia makubaliano ya kuongeza Wazee/wakongwe kwenye Tasnia ya Muziki ili waweze kuwasaida kwenye Ushauri ndani ya Shirikisho,pia watakuwa wanashiriki Vikao vya Bodi.
Wazee hao ni.Mzee Mapili, Juma Ubao, Thobias Chidumule,Hamza Kalala.Martha Mlata (Mb) na Asha Baraka.
Pia
Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa
Shirikisho ameteuliwa Ndugu Francis
Kaswahili,Vilevile Nafasi ya Makamu wa Rais aliteuliwa Ndugu Samwel
Mbwana Braiton,Upande wa wajumbe aliongezwa Ndugu Waziri Ally.Upande wa
katibu wa Fedha aliteuliwa Ndugu Mwinyi aliteuliwa kuwa Msimamizi
maswala ya Fedha."Amesema Mwasongwe.
Kubwa
zaidi Shirikisho la Mziki limeomba Kwakuwa Kundi la Mziki kwa sasa ni
Kubwa sana Nchini,Ripoti ya BASATA Mwaka 2006 ilisema zaidi ya watu
Milioni 6 Nchini wanajishughulisha na Mziki,Hivyo hadi sasa idadi
itakuwa imeongezeka sana.Shirikisho linaomba Katiba pia itamke kuhusu
haki Miliki hususani kazi za Muziki ili Wasanii wapate stahiki za kazi
zao sawa sawa na wanavyojituma kwenye kazi hiyo.Sheria itamke wazi
adhabu kali inayopaswa kutokewa kwa wezi wa Kazi za Wasanii wa Muziki.
Vile
vile Shirikisho linaomba Serikali isapoti shirikisho la Mziki kama
inavyosapoti Vyama vya Michezo mingine Nchini,Pia serikali iwaandalie
Semina ya kuwajengea uwezo wasanii "Capacity Bulding".

Mwisho,Shirikisho
linaomba sana Wasanii Washikamane na Washirikiane kurudi kwa Jamii
kutoa mkono wao kwa Jamii wanayoitumikia "Giving Back to the
Society".Hivi karibuni tunategemea kuanza kampeni yetu ya Kuokoa Mama na
Mtoto hususani Mahospitalini kwa kuchangia Vitanda,Vyandarua n.k.Hivyo
Shirikisho linaomba wasanii wote washiriki kwenye kazi za kijamii ambazo
shirikisho litaanza kuzifanya muda si mrefu.
Akijibu Swali la Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi kuhusu Msimamo wa shirikisho Kuhusu Muundo wa Serikali kwenye Katiba Mpya,Ndugu Addo Novemba amesema Shirikisho sio Chama Cha siasa na Shirikisho halina Kauli yoyote kuhusu Muundo wa Serikali kuwa iwe Moja,Mbili au Tatu.Lakini kwa mtu mmoja mmoja binafsi tunaweza kuwa na Mawazo yetu.Kwa Upande wa Addo Novemba binafsi anasema ni bora serikali Moja kuliko Kuongeza Serikali ya tatu wakati hizi mbili bado bajeti yake kama Nchi hatujaweza kuimudu.Haitakuwa afya kutatua tatizo la serikali mbili kwa kuongeza Serikali ya tatu,Kuongeza serikali ya tatu ni kuwatwisha Mzigo Watanzania usiokuwa na tija,Kuna Huduma za Afya,Miundo mbinu n.k havijatengemaa,tuanze kuongeza bajeti ya serikali ya tatu ya nini???.
Picha/maelezo na Sanga Festo wa Habari kwanza Media/Blog
No comments:
Post a Comment