ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 24, 2014

UTNC AND DICOTA DINNER WITH HON. AMBASSADOR MULAMULA NORTH CAROLINA YAFANA

Meza kuu kutoka kushoto ni Dr. Lyungai Mbilinyi (mwakilishi DICOTA), Geofrey Lipana (mwenyekiti UTNC), Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula na Matilda Tarimo Mwenyekiti Jumiya ya kimama North Carolina wakijumuika pamoja katika kumkaribisha Balozi na kufungua KICK-OFF ya DICOTA CONVENTION itakayofanyika North Carolina mwaka huu kwenye mwezi October kuanzia tarehe 2 mpaka 5 hafla hiyo ilifanyika siku ya Jumamosi March 22, 2014 katika Hotel ya Hilton Hillsbbro road, Durham, North Carolina.
Nassor Bassalama akimkaribisha Mh Balozi  ili aongee na Watanzania wa North Carolina.

Mhe. Liberata Mulamula akiongea na Watanzania wa North Carolina kwa kuwashukuru kwa kumkaribisha North Carolina huku akiwasisitizia umoja wa kuwa pamoja na jumuiya zingine hapa Marekani na kuwekea msisitizo wa ushiriki kwenye siku ya DICOTA na umuhimu wa kulipa ada kwenye Jumuiya za Watanzania ili ziendelee kudumu pia aliwaasa kuwa raia wema na kufuata msingi ya sheria ya nchi wanaoishi na kupongeza Watanzania wa NC kwa jitihada zao za maendeleo hasa kwa kujiajili wenyewe kwa kutolea mfano chuo cha Mount Eagle College kinachomilikiwa na Mtanzania
 Geoffrey Lepane akiongea machache na kumshukuru Balozi Liberata Mulamula kwa kukubali mwaliko wao na kuja North Carolina kujumuika nao.

Mwakilishi wa DICOTA, Dr. Lyungai Mbilinyi akimshukuru Balozi kwa kuja North Carolina mahali kutakapofanyika DICOTA mwaka huu na kuielezea DICOTA kwenye hafla hiyo pia alishukuru Jumuiya ya Watanzania North Carolina hasa mwenyekiti wake kwa kukubali kuwa wenyeji wa DICOTA October 2-5, 2014.

Watu mbalimbali waliotunukiwa vyeti wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe, Balozi Liberata Mulamula.

Mshereheshaji Teddy akifanya vitu vyake.

Watanzania wa North Carolina wakijumuika pamoja na Balozi Mhe. Liberata Mulamula katika ukumbi wa Hilton Hotel, Durham, NC.

David Mushi akiongelea kampuni yake ya GEEKSPlus
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
 Flora akionyesha Vazi lake by DEDA FASHION
 Mh Balozi Mulamula akipokea zawadi kutoka kwa DEDA FASHIONS

 Mh Balozi akipokea moja ya zawadi alizopewa kutoka UTNC
 Mr Rodgers Exports akionyesha cheti chake alichopokea kutoka kwa Mh Balozi Mulamula

wageni wakisimama na kuimba Tanzania Tanzania
 Hii ndio kamati iliyopokea vyeti kutoka kwa Mh Balozi
Hawa ni Models wa Deda Fashion Kwenye Ukodak
Tiana Huyu Model ndiye aliye Funga kazi
Mshereheshaji Talkia akiwa kazini





 Dj B alizungusha santuri katika ghafla hii

No comments: