ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, March 22, 2014

UVCCM WAZINDUA MBIO MAALUM ZA PIKIPIKI KUHAMIASISHA UZALENDO MIONGONI MWA VIJANA LEO MKOANI DODOMA


Leo Tarehe 22/03/2014 katika Manispaa ya Dodoma, Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), tumezindua mbio maalum za pikipiki zenye lengo la kuhamasisha uzalendo miongoni mwa vijana na kuibua fursa zinazopatikana maeneo mbalimbali ya Tanzania.

Mbio hizi maalum zimezinduliwa na Rais waAZanzibar, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mheshimiwa Dr. Ali Mohamed Shein, katika hafla fupi ya kufana iliyofanyika katika makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa Dodoma.

Mbio maalum za pikipiki zitazunguka nchi nzima na zitahitimishwa rasmi kwa matembezi ya miguu kuanzia Kibaha Mkoani Pwani hadi Dar es Salaam tarehe 25/04/2014 yatakayopokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Mrisho kikwete katika ukumbi wa Nyerere Convention. 
Kauli Mbiu Yetu

"MIAKA 50 YA MUUNGANO; VIJANA TUDUMISHE MUUNGANO WETU NA TUTUMIE FURSA ZILIZOPO KULETA MAENDELEO YETU"
TANZANIA KWANZA, MENGINE BAADAYE

Imetolewa na;
Paul C. Makonda 
Katibu wa Hamasa uhamasishaji UVCCM

No comments: