ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 13, 2014

WATANZANIA WA NEW YORK WAUAGA MWILI WA MAREHEMU AUNT LULU MWALUKO TAYARI KWA SAFARI YA MOSHI TANZANIA

Familia ya marehemu ikiwa imesimama pembezoni mwa mwili wa mama yao mpendwa Lulu Mwaluko aliefariki siku ya Tarehe 7 mwezi wa 3 katika hospitali ya Calvary iliyopo Bronx NY alikokuwa amelazwa kutokana na ugonjwa wa saratani. Watanzania wa New York pamoja na Balozi Tuvako Manongi, Mwakilishi wa kuduma wa Tanzania kwenye Umoja wa mataifa walijitokeza katika kuuaga mwili wa marehemu hapo Camelot Funeral Home Mt Vernon NY siku ya Jumamtano March 12, 2014.
Watoto wa marehemu katika picha ya pamoja siku ya kuaga mwili Jumatano March 12, 2014 Camelot Funeral Home huko Mt Vernon NY. Mwili wa marehemu utasafirishwa Alhamisi March 13, 2014 kuelekea Moshi Tanzania kwa mazishi.
Mtoto mkubwa wa marehemu akitoa shukrani kwa watu waliojitokeza kuuaga mwili wa mpendwa mama yao
Mmoja wa familia ya marehemu akiongea jambo.
Katibu wa Jumuiya ya Watanzania New York bwana Mhella akiongea kwa niaba ya jumuiya.
Dr Temba akiongea juu ya jinsi alivyo mfahamu marehemu.
Balozi akitafakari jambo
Afisa wa Ubalozi New York Mama Rose alikuwepo sambamba na Watanzania wengine.
Balozi akibadirishana mawazo na Mwenyekiti wa tawi la CCM New York Shekhe Mafutah.
Balozi akipata picha ya pamoja na wanafamilia wakiwemo viongozi wa Jumuiya ya New York, wapili toka kilia ni mdogo wa marehemu alitoka Tanzania kuja kumuuguza dada yake, Kwa picha zaidi bofya soma zaidi

No comments: