KESI
ya mauaji inayomkabili mfanyabiashara maarufu Marijan Abubakar ‘Papa
Msofe’ na mwenzake imeendelea kupigwa kalenda, baada ya upande wa
mashitaka kudai upelelezi haujakamilika.
Pia, umedai jalada la kesi hiyo lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP) na kesi itatajwa Machi 25, mwaka huu.
Msofe na Makongoro Nyerere wanakabiliwa na kesi ya mauaji ya Onesphory
Kitoli, jana walifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya
Hakimu Mkazi Hellen Riwa.
Wakili wa Serikali Leonard Challo alidai upelelezi wa kesi hiyo bado
haujakamilika na jalada la kesi hiyo liko kwa DPP kwa hatua zaidi.Msofe
na mwenzake walirudishwa rumande.
KESI
ya mauaji inayomkabili mfanyabiashara maarufu Marijan Abubakar ‘Papa
Msofe’ na mwenzake imeendelea kupigwa kalenda, baada ya upande wa
mashitaka kudai upelelezi haujakamilika.
1 comment:
Bora wasitoke kabisa maana hata mjini kumetulia utapeli na ufuska wao hauonekani tena hongera sana mahakama ya kisutu funga maisha huyo mjinga bora na hao wazungu wakiokuwa wanataoeliwa waje wajiunge na kesi
Post a Comment