ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 13, 2014

KESI YA MAUAJI INAYOMKABILI PAPAA MSOFE YAZIDI PIGWA KALENDA, ARUDISHWA TENA RUMANDE


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj12AAjv5O3GdRBSi7797dRbq0DYRoTXHwCsxdBbtGFJYMi2-qf2ja0jv1UfiSzf6qBePuj1lPgW2_-K4Sw1Zgf_807Xy2J_7AYHt-d3nIlw4QcX3P-4Ay2mFElHucb4scwvpeu_MEaxvk/s1600/PAPAAMSOFE3.jpgKESI ya mauaji inayomkabili mfanyabiashara maarufu Marijan Abubakar ‘Papa Msofe’ na mwenzake imeendelea kupigwa kalenda, baada ya upande wa mashitaka kudai upelelezi haujakamilika.
Pia, umedai jalada la kesi hiyo lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP) na kesi itatajwa Machi 25, mwaka huu.
Msofe na Makongoro Nyerere wanakabiliwa na kesi ya mauaji ya Onesphory Kitoli, jana walifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Hellen Riwa.
Wakili wa Serikali Leonard Challo alidai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na jalada la kesi hiyo liko kwa DPP kwa hatua zaidi.Msofe na mwenzake walirudishwa rumande.

1 comment:

Anonymous said...

Bora wasitoke kabisa maana hata mjini kumetulia utapeli na ufuska wao hauonekani tena hongera sana mahakama ya kisutu funga maisha huyo mjinga bora na hao wazungu wakiokuwa wanataoeliwa waje wajiunge na kesi