![]() |
| Mchungaji Joel Osteen, kiongozi wa kanisa la Lakewood la nchini Marekani. |
Watu wasiofahamika wameiba pesa za michango kiasi cha shilingi dola laki
sita (600,000) za Marekani pamoja na hundi katika kanisa la Lakewood la
nchini Marekani linaloongozwa na mhubiri maarufu Joel Osteen jumapili
iliyopita. Awali wizi huo aukutambuliwa mpaka pale mfanyakazi wa zamu
aliyetambuliwa kwa jina la Harris County Sheriff's alipofika kanisani
hapo siku ya jumatatu saa mbili na nusu asubuhi na kugundua uvunjifu na
upotevu huo.
Kanisa hilo limetaka mtu yeyote aliyehudhuria ibada kanisa hapo siku ya
jumapili awe makini na akaunti yake ya benki na endapo atagundua jambo
lolote lenya ualakini katika akaunti yake basi atoe taarifa haraka
iwezekanavyo. Kanisa hilo limewatoa wasiwasi waumini wake kwamba kitendo
hicho kisitafsiriwe kwamba kanisa linavujisha taarifa zao bali sadaka
hizo zilikuwa za mchango maalumu uliokusanywa wiki iliyopita.
"Tunafanya kazi na polisi kwa ukaribu kushughulikia tukio
lililojitokeza", taarifa ya kanisa ikiwa imenukuliwa hivyo, mchango huo
tayari ulikuwa una bima hivyo wanaangalia utaratibu na kampuni ya bima
ili warudishiwe fedha zilizoibiwa kwa kanisa. Mchungaji Joel ni kati ya
wachungaji ambao wanapitia majaribu ya kusemwa vibaya ikiwa pamoja na
watumishi wenzie huku pia akihusishwa kuabudu vitu tofauti na Mungu,
kubwa zaidi inadaiwa huwa ataji Yesu mara nyingi kwenye mafundisho yake.
Lakini licha ya hayo yote huduma yake imekuwa ikihudhuriwa na watu
takribani 45, 000 kila wiki.
![]() |
| Sehemu ya kanisa la Lakewood linavyoonekana kwa ndani, Joel akiwa madhabahuni akifundisha.©Lakewood church. Chanzo : Charisma. |


1 comment:
maskini joel ostein nampenda sana mahubiri yake na hajalishi kama hahubiri yesu,anachofanya ni sawa kuwapa watu amani ya moyo ya kweli na ku wa uplift self esteem zao mungu amsadiye sana na kanisa lake
Post a Comment