Kijana, Andrea John (26) akiwa na mguu ulioota magamba mithili ya mti mkavu.AMA
KWELI HUJAFA HUJAUMBIKA! Kijana, Andrea John, 26, amejikuta katika
wakati mgumu mara baada ya kupatwa na ugonjwa wa ajabu uliosababisha
mguu wake kuwa na magamba mithili ya mti mkavu.
Andrea
anayeishi kwa mateso makali maeneo ya Argentina, Manzese jijini Dar,
anasema mwaka 2005 akiwa anafanya kazi katika mashine ya kusaga na
kukoboa, alijikuta akianza kuumwa na vidole vya mguu wa kulia na baadaye
maumivu hayo kuhamia kiunoni, kitu kilichomfanya kukosa raha.
Anaendelea kusimulia: “Mara baada ya kusikia maumivu ya vidole na kiuno, nilikwenda katika Hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Anaendelea kusimulia: “Mara baada ya kusikia maumivu ya vidole na kiuno, nilikwenda katika Hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
“Nilipofika
huko, wakaamua kuchukua vipimo vya damu kwa ajili ya uchunguzi lakini
hawakutaka kunipa majibu, nilishangaza sana kwa sababu sijawahi kuona
kitu kama hicho.
KUFIWA NA MKE
“Mwaka 2006 nilifiwa na mke wangu, Nuru Kassim ambaye ameniachia mtoto mdogo, Agness mwenye umri wa miaka 7. Hilo lilikuwa pigo kubwa kwangu.
“Mwaka 2006 nilifiwa na mke wangu, Nuru Kassim ambaye ameniachia mtoto mdogo, Agness mwenye umri wa miaka 7. Hilo lilikuwa pigo kubwa kwangu.
“Kutokana
na matatizo ya kuugua nilishindwa kumlea mtoto wangu hasa ikizingatiwa
kuwa sikuwa nafanya kazi, bahati nzuri mwanamke mmoja wa Kiarabu
alijitokeza na kuamua kumchukua Agness na kuishi naye,” alisema Andrea
kwa masikitiko.
Aliongeza
kuwa aliendelea kupata matibabu japokuwa hayakubadilisha kitu chochote
zaidi ya mguu wake kuanza kuota magamba ambayo yaliufanya kubadilika na
kufanana na mti uliokauka. Baada ya kuona hali imekuwa hivyo na maumivu
yakimzidia kila siku, aliamua kurudi Hospitali ya Mwananyamala ambapo
walimwambia achukuliwe vipimo kwa mara nyingine.
KUHAMISHIWA MUHIMBILI
“Kilichofanyika ni kuchukuliwa vipimo kwa kutumia kipimo cha kupimia saratani ya ngozi ambacho hujulikana kitaalamu kama Biopsy na hivyo kukutwa na ugonjwa wa kansa ya ngozi uitwao Kaposis Sarcoma,” alisema.

Alisema hakuweza kupatiwa matibabu zaidi ya kuandikiwa karatasi ya kuhamishiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar.
Alipokuwa
Muhimbili, Andrea alilazwa kwa muda wa miezi miwili bure kutokana na
kutokuwa na uwezo kifedha, madaktari waliliangalia tatizo lake kiundani
na wakashauri asikatwe mguu hivyo wakamuandikia dozi ya dawa za vidonge
na kumruhusu kurudi nyumbani.
Mpaka
sasa Andrea anaendelea na vidonge hivyo na hana msaada wowote zaidi ya
kutembea mtaani na kuomba chochote japo apate chakula cha siku na
anashindwa kurudi hospitali kwa kuwa hana hata senti tano.
Andrea
anaomba msaada kwa yeyote aliyeguswa na habari hii ili aweze kupata
fedha za kuendeleza matibabu yake na kujikimu. Kutoa ni moyo na
ukimsaidia utapata baraka za Mungu. Unaweza kuwasiliana naye kupitia
namba ya dada yake. Zainabu John Kimweri – 0656 037075.
-GPL
No comments:
Post a Comment