Mhe. Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Ubalozi Mdogo wa Tanzania uliopo Dubai, akiwa katika picha na Mhe. Yousef A. Rahmani Al Mahaira, Mkurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya UAE, Ofisi ya Dubai baada ya kikao chao leo ofisini kwa Mhe. Yousef. Kikao chao kilijadili maandalizi ya maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanzania. Mhe. Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu na Mtukufu Sheikh Ahmed Bin Saeed Ak Maktoum, Rais wa Idara ya Anga ya Dubai na Mwenyekiti wa Shirika la Ndege la Emirates watakuwa wageni rasmi. Sherehe hizo zitafanyika tarehe 14 Aprili katika Hotel ya Le Meridien Dubai.
Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai Mhe. Omar Mjenga, amtembelea ofisini kwake Mhe. Kariuki Mugwe, Balozi Mdogo wa Kenya, Dubai
Wakiwa katika mazungumzo na kubadilishana mawazo kuhusu njia wanazotumia kuvutia wawekezaji na utalii. Mhe. Kariuki alimueleza Mhe. Mjenga njia wanazotumia kuwatafutia kazi wananchi wao. Kwa sasa Tanzania imeweka mkakati wa kuhakikisha Watanzania wengi wanapata kazi Dubai
Waheshimiwa wakiwa katika picha baada ya mazungumzo.



1 comment:
sikufahamu kama Bwana Mjenga ni Balozi Mdogo.
Post a Comment