
Flaviana Matata, Herriet Paul na Simone Awor, wawakilisha East Africa Kwenye African TOP
Kuna uwezekano mkubwa sana kuweza kuwafamu MODELS wakubwa wa AFRIKA kama African Fashion Models Alek Wek , Ajuma Nasenyana , Oluchi Onweagba au Liya Kebede ambaowameweza kung’ara, kupata mafanikio makubwa sana na kufanya Afrika kuwa kwenye ramani ya dunia ya Fashion.
Flaviana Matata (Tanzania) ambae yupo chini ya Agency ijulikanayo kama WILHELMINA iliyopo NEW YORK, Herriet Paul (Tanzania) ambae yupo chini ya WOMEN MODEL Management iliyopo NEW YORK na Simone Awor (Uganda) chini ya ICE MODEL Management mjini CAPE TOWN. Hawa ni models kutoka EAST AFRICA ambao wamefanikiwa kuingia kwenye TOP 20 African Models wanaojulikana na wenye uwezo mkubwa na ambao wanaiendesha dunia ya hivi sasa kwenye upande wa Fashion.
Taarifa hizi zinetolewa na tovuti ijulikanayo kama abidjanaise.blogspot.com ambao wameweza kutambulisha kila sura ya models hao 20 wakiwemo warembo hawa wa Tanzania na Uganda ambapo wengi katika models hao wa kike ni kutoka nchi jirani ya SUDAN na kuweka Kicha cha habari “Top 20 African Fashion Models (You Need to Know)”CREDIT:GONGAMIX


1 comment:
Flaviana huo mdomo umeunguza na nini mwanangu, unajua mambo yanaponoga ukijifanya kunogesha zaidi ndio mwanzo wa kuharibu hata mchuzi wenyewe. Hebu tuliza boli unatuonyesha staha tofauti mmhhh..
Post a Comment