KATIBU MKUU WA CCM,KINANA AWASILI SALAMA MKOA WA KATAVI USIKU WA KUAMKIA LEO AKITOKEA KIGOMA.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia kwa ufupi wakazi wa mji wa Karema
mkoani Katavi usiku huu mara baada ya kuwasili akitokea mkoani Kigoma
kwa boti na kusafiri nayo ndani ya ziwa Tanganyika takribani kwa masaa
kumi na manne.Kutokana na safari hiyo kuwa ndefu ya majini,inaelezwa
kuwa kuna baadhi ya Watu wamedai msafara wa Katibu Mkuu huyo,Kinana
umepotewa ziwa la Tanganyika,jambo amabalo si la kweli na la kizushi.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwapungia wenyeji wake (hawapo pichani)
waliofika kumpokea usiku huu kwa boti akitokea mkoani Kigoma katika
bandari ya Karema mkoani Katavi,ambako amemaliza ziara yake ya siku tano
na kuhamia mkoani Katavi ambako pia atakuwa na ziara ya siku nne.
Mkuu wa
Mkoa wa Kigoma Kanal Mstaaf Issa Machibya akishuka kwenye boti usiku huu
kwenye bandari ya Karema mkoani Katavi akiwa ameambatana na Katibu Mkuu
wa CCM,Ndugu Kinana,na Viongozi wengine wa Taifa,Mkoa na Wilaya tayari
kwa kuanza ziara ya siku nne mkoani Katavi.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishuka kwenye boti wakati wenyeji wake
(hawapo pichani) walipokuwa wakimsubiri kumpokea usiku huu akitokea
mkoani Kigoma katika bandari ya Karema mkoani Katavi,ambako amemaliza
ziara yake ya siku tano na kuhamia mkoani Katavi ambako pia atakuwa na
ziara ya siku nne.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipokelewa na Viongozi mbalimbali wa mkoa na
Wilaya ndani ya Mkoa wa Katavi usiku huu,alipokuwa akiwasili kwenye
bandari ya Karema mkoani humo usiku huu.Kinana ameongoza na Katibu Wa
NEC,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye,Mjumbe wa NEC,Balozi Ali Karume,Mkuu wa
mkoa wa Kigoma,Kanal Issa Machibya,Mwenyekiti wa CCM,Mkoa wa Kigoma
ndugu Kabouru na wengineo.
Kinana akipokelewa na Gwaride la chipukizi usiku huu ndani ya mkoa wa Katavi.
No comments:
Post a Comment