Akizungumza jana na waandishi wa habari mjini Dodoma, mwakilishi wa kundi hilo Profesa Ibrahim Lipumba alisema kuwa katika kikao chao wamekubaliana kuzunguka nchi nzima kufanya mikutano ya hadhara kwa wananchi kwa kuwajumuisha wajumbe wasiokuwa na dharura.
“Tumekubaliana kwamba siku ya Jumamosi kwa pamoja Wabunge wote ambao hatuna dharura tukuwa tumeenda Zanzibar, kutakuwa na mkutano wa hadhara kuanzia saa nne asubuhi. Tutaondoka na siku hiyo na Boti ya saa moja asubuhi kuelekea Zanzibar. Katika mkutano wa Zanzibar tutaeleza yaliyojiri katika Bunge hili Maalumu....” alisema Lipumba kama anavyosikika kwenye video iliyopachikwa hapo chini.
Viongozi wa Ukawa walotoka nje ya Bunge Maalum jana wakipinga jinsi mjadala wa Katiba Mpya unavyokwenda, na kudai kuwa hawako tayari kurudi Bungeni humo wiki ijayo, wala hawatarejea kwenye kikao cha Agosti, endapo hawatahakikishiwa kuwa maudhui yaliyomo ndani ya Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya yatajadiliwa kama yalivyo.
No comments:
Post a Comment