Advertisements

Thursday, April 24, 2014

MIPAKA YA HAUSIGELI NDANI YA NYUMBA -2




TUKO ndani ya kumalizia Sikukuu ya Pasaka, lakini moyo wangu utakuwa safi kama sikukuu hii itapita huku nikiwa nimetoa la moyoni kuhusu maisha ya wanandoa wa siku hizi.Ninaposema wanandoa namaanisha watu wawili wa jinsi tofauti wanaoishi kama mume na mke ndani ya nyumba moja.

Katika miaka ya hivi karibuni, kimjinimjini familia nyingi zinazojiweza zimekuwa zikiajiri wasichana wa kazi (mahausigeli) kwa ajili ya kuwasaidia kazi za ndani, hilo si baya, inakubalika. Lakini hausigeli ndani ya nyumba ana mipaka yake.

HAUSIGELI, BAADAYE MAPENZI
Lakini baadhi ya familia hizo, wasichana hao wa kazi wamekuwa ndiyo chanzo cha ndoa kuvunjika kama siyo kuparaganyika kwa madai kwamba, akina baba wengi hujikuta wakinasa kimapenzi kwa mahausigeli hao.

Nilipata bahati ya kuzungumza na baadhi ya akina baba waliowahi kuangukia kwenye penzi la siri na wasichana wa kazi mpaka ndoa zao kuyumba, walisema tatizo ni kishawishi cha ukaribu!

HAUSIGELI KUWA MTU WA MWISHO
Kikubwa ambacho nilikibaini kuhusu madai ya kuwepo kwa ushawishi wa ukaribu ni kitendo cha baadhi ya wanafamilia, hasa mke ndani ya nyumba kumpa hausigeli kazi ya kumfungulia mlango baba mwenye nyumba endapo atakuwa amechelewa kurudi.

HAUSIGELI NA CHAKULA CHA BABA
Si kufungua mlango tu, akina mama wengi, ukifika muda wa kulala, kazi ya kuandaa chakula cha ‘baba’ huwa ni ya msichana wa kazi. Yeye ndiye ajue maji ya kunywa yapo, sabuni ya kunawia ipo, matunda yapo, nyongeza ya chumvi inafanyika vizuri endapo baba mwenye nyumba atahitaji wakati wa kula. 

HAUSIGELI NA MILANGO YA NYUMBA
Kama msichana wa kazi atamfungulia mlango baba, haina ubishi ndiye atakayefunga na kuanza kumwandalia chakula.

Kwa hesabu za harakaharaka mpaka hapo, hausigeli anakuwa mtu wa mwisho kwa siku kukutana na baba mwenye nyumba.

MADHARA YAKE 
Madhara ya utaratibu huu ni kuibuka kwa mazoea yasiyokuwa na sababu yoyote, kama vile baba mwenye nyumba kutaniana na msichana wa kazi.

Msichana wa kazi kujenga mazoea ya kumwomba baba mwenye nyumba fedha za mahitaji yake madogomadogo kama mwanamke (yanajulikana) ambayo anapomweleza mama mwenye nyumba humwambia asubiri mshahara wake mwisho wa mwezi. 

HAUSIGELI HUTUNZA SIRI KULIKO MKE 
Utafiti unaonesha kwamba, msichana wa kazi anapozoeana na baba mwenye nyumba na kupewa vijisenti vya kujikimu, hana haja ya kuambiwa asiseme kwa mama mwenye nyumba bali mwenyewe anajua wajibu wake ni kutokusema ili ‘kutuzwa’ huko kuendelee kila wakati wa uhitaji unapofika.

Wengi wanasema wake zao si watunza siri kama mahausigeli.
Akina baba wengi waliozungumza na safu hii, walikiri kwamba mara mazoea ya msichana wa kazi na baba yanaponoga na kufikia hatua ya kumpa pesa za matumizi,

basi msichana wa kazi hawezi kununua kitu kikubwa mpaka anapopata mshahara wake wa mwisho wa mwezi na kama atanunua, mfano nguo, kuzivaa ni mpaka pale anapopokea mshahara unaotambulika.

Lengo ni kwamba, atakapoonekana na nguo mpya iwe rahisi kuaminika na mama mwenye nyumba kwamba mshahara wake ndiyo umefanya kazi hiyo.

Kama utapitia kwa umakini tangu mwanzo wa makala haya utabaini kwamba, yote niliyoyaandika yanatokana na akina mama wengi kuwapa majukumu makubwa wasaidizi wao wa ndani na hivyo kuwa ndiyo wenye nyumba na wao kuwa wasaidizi. Inachekesha sana! Huu ni ubishoo wenye kuleta madhara
.Cridit:GPL

No comments: