Advertisements

Wednesday, April 23, 2014

MJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA ATISHIWA KUUAWA

Mjumbe wa Bunge la Katiba kutoka Zanzibar, Nassoro Salum Ali, amedai kuwa amekuwa akitishiwa kuuawa kutokana na msimamo wake wa kutaka muundo wa serikali mbili.
Ali ambaye pia ni mjumbe katika Baraza la Wawakilishi (CCM), alitoa madai hayo bungeni, wakati akichangia mjadala unaohusu sura ya kwanza na ya sita ya Rasimu ya Katiba.

Alidai kuna watu Zanzibar ambao wanaendekeza ubaguzi, hawataki umoja, amani na wanahamasisha utengano, jambo ambalo amesema hakubaliani nalo na yupo tayari kufa kusimamia msimamo wake.

Alisema amekuwa akipata wakati mgumu kutoka kwa baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ambao humpa vitisho mbalimbali ikiwamo kuuawa kutokana na msimamo wake wa kupinga ubaguzi na kutetea muungano.

“Jimbo ninaloongoza lina watu wengi mchanyiko kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, lakini wanaishi kwa amani na kushirikiana hatubaguani wala kuishi kwa chuki….tatizo kuna watu wanajiona ni Waarabu zaidi, lakini mbona mimi pia nina asili ya kiarabu, lakini sina mambo hayo?” alihoji na  kuongeza:

“Mimi siogopi kuuawa kwani atakayeniua na yeye atakufa…na siku mkisikia nimeuawa mjue kuna chama kimoja kinahusika.”

1 comment:

Anonymous said...

Tanzania chukua tahadhari- Kulazimisha serikali tatu kunani?