Kocha Msaidizi wa Yanga,Boniface Mkwasa.
Ahadi zisizotekelezeka za viongozi wa soka nchini, zimekuwa zikichangia kuyumba kwa klabu kubwa nchini na Kocha Msaidizi wa Yanga, Boniface Mkwasa, amesema umefika wakati sasa klabu hizo kusajili wachezaji wenye kuweka mbele uzalendo kuliko maslahi yao.
Kauli hiyo ya Mkwasa imefuatia baadhi ya wachezaji wa kigeni akiwamo Mganda, Emmanuel Okwi, kudaiwa kuikacha timu mpaka pale atakapolipwa kiasi cha Dola za Marekani 50,000 za usajili ambazo anaidai timu hiyo.
Akizungumza na gazeti hili jana, Mkwasa, alisema kuwa wachezaji kutokuwa na uzalendo na mapenzi ya kweli na timu ni moja ya sababu zilizoifanya Yanga ishindwe kutetea ubingwa wake msimu huu licha ya kusajili nyota mbalimbali wenye viwango vya juu.
Mkwasa alisema hali hiyo iliyotokea msimu huu uliomalizika iwe fundisho kwa viongozi na kutorudia makosa hayo kwenye maandalizi ya msimu ujao.
"Ni lazima tusajili wachezaji ambao wataweka mbele uzalendo na si kuangalia maslahi, mchezaji anatakiwa awe na mapenzi na timu ndiyo ataitumikia kwa moyo," alisema Mkwasa ambaye aliwahi kuichezea timu hiyo na kikosi cha taifa (Taifa Stars).
Alieleza kuwa tayari wameshaandaa ripoti ya benchi la ufundi na uzalendo ni moja ya vigezo ambavyo mchezaji atakayesajiliwa anatakiwa kuwa navyo.
"Tunajipanga upya kwa ajili ya msimu ujao, kuna mambo mengi tumeyaona na tutayafanyia kazi, mimi (Mkwasa) sikuwapo katika mzunguko wa kwanza hivyo niliipokea timu iliyokuwa imeshasajiliwa," kocha huyo aliongeza.
Aliwataka wachezaji wa timu hiyo kutumia vyema mapumziko ili watakaporejea tena kuanza maandalizi ya msimu ujao wawe na nguvu na kasi mpya.
Hata hivyo, tuhuma za ubabaishaji miongoni mwa viongozi wa klabu nyingi za Tanzania umetajwa kuwa sababu ya viongozi kushindwa kuwadhibiti kitabia wachezaji wao kwa kujua kwamba kuna ahadi nyingi wanazowapa kisha wanashindwa kuzitekeleza.
Yanga imemaliza msimu huu wa ligi wa mwaka 2013-14 ikiwa ya pili na kukata tiketi ya kuiwakilisha Tanzania Bara katika mashindano ya Kombe la Shirikisho mwakani.
Kikosi hicho cha Jangwani pia kitapeperusha bendera ya Bara kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) yatakayofanyika mwezi Agosti mwaka huu hapa nchini.
Azam ya jijini ndiyo timu iliyoibuka mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Bara kwa mara ya kwanza tangu ilipoanza kushiriki ligi hiyo msimu wa mwaka 2008-09.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment