Mwakilishi wa Jimbo la Kiembe Samaki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (katikati) wakiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Jimbo la Kiembe samaki Ramadhan Mrisho wa kushoto, kulia Mwenyekiti wa Kamati ya michezo ya Jimbo hilo Juma Abdul-rabi kabla ya kukabidhi pesa taslimu na vifaa vya michezo kwa timu za Jimbo hilo ikiwa ni ahadi aliyoitoa wakati wa kampeni zake hafla hiyo imefanyika katika Hoteli ya Ocean View Mjini Zanzibar.
Diwani wa Jimbo la Kiembe Samaki, Bw. Gharib Mohamed Addy akizungumza na wanamichezo wa Jimbo hilo (hawapo pichani) kabla ya kukabidhiwa vifaa vya michezo na Mwakilishi wa Jimbo la Kiembe samaki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo.
Baadhi ya wanamichezo na viongozi mbalimbali wa Jimbo la Kiembe Samaki wakimsikiliza Mwakilishi wa Jimbo hilo Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (hayupo pichani) kabla ya kukabidhi pesa na vifaa vya michezo kwa timu za Jimbo lake.
Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akimkabidhi pesa shilingi laki nne kiongozi wa timu ya Smoll Zico ya Kiembe Samaki ikiwa ni ahadi aliyoitoa wakati wa kampeni zake.
Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akimkabidhi Katibu wa Timu ya Mbweni Kids Khalifa Khamis vifaa mbalimbali vya michezo, Jumla ya timu nane za jimbo hilo zimepata pesa na vifaa mbalimbali vya michezo vyenye thamani ya shiling milioni saba na nusu.
(PICHA NA MAKAME MSHENGA WA MAELEZO ZANZIBAR)
No comments:
Post a Comment